WAITARA AMPELEKA WAZIRI WA MIFUGO PUGU MNADANI
Hivi karibuni Mbunge wa jimbo la Ukonga amefanya
ziara mnada wa ng'ombe na Mbuzi uliopo Kata ya Pugu Station akiwa
ameongozana na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina
Lengo la ziara hiyo ni kujua changamoto
zilizopo kwenye mnada wa Mifugo Pugu pamoja na kutambua mipaka ya eneo la mnada
sehemu lilipopakana na wananchi
Viongozi walioongozana na Waziri wa Mifugo katika
ziara hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo Dr.Mary Mashingo, Dr. Asimwe Ruiguza,Afisa wa minada wa Wizara ya Mifugo,Dr.
Basil na Mkuu wa mnada wa Pugu,Kerambo Samwel
Huu ni mwendelezo wa Mbunge kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wapiga kura
wake wa Ukonga kwani baada ya ziara Wazara wa Mifugo ameahidi kutatua kero ya maji
iliopo katika mnada huo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara
(wapili kushoto) akiongozana na Waziri ya Mifugo, Luhaga Mpina (wapili kulia)
baada ya kuwasili katika mnada wa Mbuzi na Ng`ombe uliopo Pugu Station jijini
Dar es Salaam hivi karibuni.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akiteta jambo na Waziri ya
Mifugo, Luhaga Mpina wakati wakikagua mipaka ya eneo la mnada sehemu
lilipopakana na wananchi wa mtaa Bangulo Kata ya Pugu Station.
Waziri ya Mifugo, Luhaga Mpina (kushoto) na Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara wakimsikiliza kwa makini mfanyabiashara wa
Mnada wa mbuzi na Ng`ombe uliopo Pugu Station baada ya kuwasili mnadani hapo
kusiliza kero zilizopo hapo pamoja na kukagua mipaka ya eneo la mnada sehemu
ulipopakana na Wakazi wa Mtaa wa Bangulo.
Baadhi ya wakazi na Wafanyabiashara waliopo
karibu na Mnada wakisikliza kwa makini hoja zinazoendelea katika ziara ya
Mbunge pamoja na Waziri wa mifugo baada ya kuwasili mnadani hapo hivi karibuni.
No comments