Breaking News

WAITARA;AWATAKA HALMASHAURI NA DAWASA WATOE TAARIFA KWA WAKAZI WA UKONGA MIRADI YA MAJI ITAKAYOFANYIKA KATIKA MWAKA HUU WA FEDHA

Na mwandishi wetu
Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara afanya ziara Jimboni akiwa ameongozana na Wahandisi wa maji toka Dawasa na Halmashauri ya Ilala 

Kata zilizofikiwa na ziara hiyo ni Kata ya Msongola,  Zingiziwa, Chanika, Buyuni Pugu Station na Pugu Kajiungeni 

Agenda kuu katika ziara hiyo ni kutatua kero ya maji Ukonga pamoja na kufufua miradi ya maji ambayo ilishakuwepo na hivi sasa haifanyi kazi Mfano,pump kuharibika, kukosekana kwa umeme

Agenda nyingine ni Kuendeleza miradi ya maji ambayo ilishatekelezwa ila bado gharama kidogo ili ifanye kazi badala kuanza miradi mipya kama kuchimba visima

Vilevile Waitara alitaka Wahandisi wa Maji wa Halmshauri na Dawasa watoe taarifa za miradi ambayo itafanyika katika jimbo la Ukonga katika mwaka huu wa fedha ili apate hoja ya kwenda kusema pindi Bunge litakapoanza wiki ijayo

Wahandisi aliiongozana nao ni Mhandisi Mkuu wa maji Manispaa ya Ilala,Upendo Lugongo , Kaimu Mhandisi wa maji Manispaa ya Ilala,Kheri Sultan na  Msimamizi wa miradi ya maji ya jamii kutoka DAWASA,Charles Makoye.
Huu ni mwendelezo wa Waitara  kuendelea kutekeleza ahadi zake alizowaahidi wana wa Ukonga. 



Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (kulia) akizungumza na  madiwani,Watendaji wa kata na wenyenyeviti wa mitaa ya Kata ya Msongola jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwasili katika kata hiyo kwa ajili ya ziara ya kutatua kero ya maji iliyopo jimboni pamoja na kufufua miradi ya maji ambayo ilishakuwepo na hivi sasa haifanyi kazi huku akiwa ameongozana na Wahandisi wa maji Kutoka Halmashauri na Dawasa. Huu ni mwendelezo wa Mbunge wa Ukonga kuendelea kutekeleza ahadi zake alizowaahidi wapiga kura wake.



Diwani wa Kata ya Msongola,Azizi Mwalile (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (katikati) jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwasili katika kata hiyo huku akiwa ameongozana na wahandisi wa maji kutoka Halmashauri ya Ilala na Dawasa ili kujadili pamoja na kujua hali ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo.kulia ni Kaimu Mhandisi wa maji Manispaa ya Ilala,Kheri Sultan.



Kaimu Mhandisi wa maji Manispaa ya Ilala,Kheri Sultan(katikati) akizungumza jambo na watendaji wa kata,watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa ya kata ya Msongola katika ziara ya Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (kushoto) huku akiwa ameongozana na wahandisi hao yenye agenda ya kutoa taarifa kwa wakazi wa kata ya hiyo miradi ya maji iliyopangwa kufanywa kwa mwaka huu wa fedha.Kulia ni Mhandisi Mkuu wa maji Manispaa ya Ilala,Upendo Lugongo.



Msimamizi wa miradi ya maji ya jamii kutoka DAWASA,Charles Makoye(katikati) akitoa taarifa ya miradi ya DAWASA itakayofanyika katika kata ya Msongola kwa mwaka huu wa fedha.



Mhandisi Mkuu wa maji Manispaa ya Ilala,Upendo Lugongo akizungumza jambo jijini Dar es Salaam jana na watendaji wa kata,watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa katika ziara ya Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (kushoto) katika kata ya Msongola kujadili upatikanaji wa maji pamoja na kutoa taarifa ya miradi ya maji itakayo fanyika katika kata hiyo kwa mwaka huu wa fedha.




Baadhi wa wenyeviti wa serikali za mitaa ya Kata ya Msongola wakitoa taarifa ya changamoto za miradi maji ya iliyopo katika mitaa yao.


Diwani kata ya Chanika,Ojambi Massaburi akizungumza kitu na watendaji wa kata,watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa katika hafla ya ziara ya Mbunge wa jimbo la Ukonga huku akiwa ameongozana na wahandisi kutoka Halmashauri ya Ilala na DAWASA yenye agenda ya kujua hali ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa kata ya Chanika na Zingiziwa jijini Dar es Salaam jana.

Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akizungumza watendaji wa kata,watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa wa Kata ya Chanika na Zingiziwa.

Diwani kata ya Zingiziwa,Hussein Togolo akizungumza kitu na watendaji wa kata,watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa katika hafla ya ziara ya Mbunge wa jimbo la Ukonga huku akiwa ameongozana na wahandisi kutoka Halmashauri ya Ilala na DAWASA yenye agenda ya kujua hali ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa kata ya Chanika na Zingiziwa jijini Dar es Salaam jana.


Mhandisi Mkuu wa maji Manispaa ya Ilala,Upendo Lugongo akitoa taarifa ya miradi ya maji inayotakiwa kufufuliwa miradambayo ilishakuwepo na hivi sasa haifanyi kazi kutokana na kuharibika katika kata ya Chanika na Zingiziwa ili ipunguze kero ya ukosefu wa maji katika kata hizo.



Msimamizi wa miradi ya maji ya jamii kutoka DAWASA,Charles Makoye(kulia) akijibu maswali ya kero za upatikanaji wa maji kutoka kwa watendaji wa kata,watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa ya kata ya Chanika na Zingiziwa katika ziara hiyo jijini Dar es Salaam jana.






Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa ya Kata ya Chanika na Zingiziwa wakitoa taarifa ya changamoto za miradi maji ya iliyopo iliyopo katika mitaa yao.


Mhandisi Mkuu wa maji Manispaa ya Ilala,Upendo Lugongo akizungumza jambo na viongozi wa kata ya Buyuni,Pugu kajiungeni na Pugu Station.


 Diwani kata ya Buyuni,Twaha Malate akizungumza na Mbunge wa jimbo la Ukonga,Mwita Waitara (wapili kushoto) na Wahandisi wa maji kutoka Halmashauri ya Ilala  na Dawasa baada ya kuwasili katika kata hiyo jijini Dar es Salaam jana katika ziara ya Mbunge huyo yenye agenda ya Kutatua kero za maji ni pamoja na kuendeleza visima vilivyopo badala ya kuchimba visima vingine ili kupunguza tatizo la ukosefu wa maji katika kata ya Buyuni pamoja na Pugu.
 Mtendaji kata ya Pugu,Alicia Chale akizungumza jambo na ugeni huo.

 Msimamizi wa miradi ya maji ya jamii kutoka DAWASA,Charles Makoye(katikati) akitoa taarifa ya miradi ya DAWASA itakayofanyika katika kata ya Buyuni,Pugu kajiungeni na Pugu Station kwa mwaka huu wa fedha.



Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa ya kata ya Buyuni,Pugu kajiungeni na Pugu Station wakitoa taarifa ya changamoto za miradi maji ya iliyopo katika mitaa yao.

No comments