Breaking News

TIGO WASAINI MKATABA MPYA AWAMU YA 8 KUPELEKA MAWASILIANO KATA 371

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali nchini Tigo imesaini  mkataba mpya wa awamu ya 8 wa kufikisha huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini kwa ushiriikiano kati ya Tigo na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) , Kwa ujumla Tigo wanatarajiwa kujenga na kuboresha minara 409 katika kata 371.

Akizungumza na Waandishi wa habari  Mkurugenzi wa kitengo cha Udhibiti Tigo, Bi. Sylivia Balwire amesema kuwa utiaji saini huo umefanywa na Mkurugenzi wa Tigo Zantel Bwn. Kamal Okba ambapo mgeni rasmi alikua ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt . Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine mbalimbali .

" Tunaongoza kwa kuchukua asilimia 33 ( 33% ) ya kata zote zitakazonufaika awamu hii , ambapo tunaenda kujenga kwenye takribani kata 371 , hii yote ni kuunga mkono jitihada za serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Mhe. Dkt . Samia Suluhu Hassan ya kukuza nakuhakikisha mawasiliano yanamfikia kila mwananchi lakini kubwa zaidi ni kwamba Tigo tumekusogezea simujanja za bei nafuu ambapo mteja atalipia Tsh. 1000 ( Elfu moja ) kwa siku" . alimalizia Bi. Sylivia



No comments