Breaking News

KIWANGO CHA SIMENTI NCHINI – UKWELI NI HUU HAPA

 

Ninaendelea kusikia na kuona mengi juu ya huu muunganiko wa kampuni za simenti na ninazidi kushangaa kwa nini kuna habari nyingi tofauti kwenye vyombo vya habari? Nimeamua kufanya utafiti kuhusu uwezo wa makampuni ya simenti Tanzania na picha yake inanivutia.

Ngoja nikwambie, kwanza nimeanza kwa kutazama hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk Ashantu Kijaji na nimesikia machache….

Alisema, wizara hiyo ilifuata sheria na kanuni zote baada ya kupokea ombi la muunganiko. Unaposoma kifungu cha 11 kifungu kidogo cha 2 cha sheria ya Tume ya Ushindani (FCC) ya mwaka 2018 pamoja na kifungu cha 1 kifungu kidogo cha 2 kinatoa vigezo kwa kampuni zinazoungana na zimekidhi vigezo vyote vilivyowekwa hapo juu ili kuwasilisha ombi lao bila kujali ombi lao la awali kukataliwa au kukubaliwa. Hii inamaanisha kuwa kampuni mpya haiwezi kuwa na zaidi ya asilimia 35 ya soko.

Tangu ombi hilo, nimekuja kujua kuwa serikali ilifanya utafiti na uchunguzi ili kuhakikisha muunganiko huo hautakuwa mbaya kwa Tanzania. Na ndo sababu waliidhinisha ombi hilo, nami nikaanza safari yangu.

Watu wengine wanasema kuwa kampuni hii mpya itatawala soko, lakini mimi binafsi silioni hilo. Nikawapigia simu marafiki wachache wanaofanya kazi viwanda vya simenti pamoja na kupitia / kusoma mitandaoni, nilipata yafuatayo na kuwasilisha kupitia jedwali lifuatalo.

Lazima niwe muwazi na kusema kwamba kiwanda cha simenti cha maweni nimewasilisha kiwango chake ambacho ni pamoja na ujenzi wa tanuru lao jipya la tani milini nne (mil 4) kwa mwaka. Nilipata taarifa hizo lakini sikuweza kupata taarifa ya tathmini ya athari za mazingira ya tanuru hilo. Nikazungumza na baadhi ya watu na kuwahoji kama wanaona tanuru likiendelea.


Uwezo wa viwanda vya Simenti Tanzania

Kampuni
Uwezo
(tani kwa mwaka)
Asilimia ya Usambazaji
Maweni Limestone (Huaxin

2,200,000
20%
Dangote Cement
2,200,000
20%

Tanzania Portland Cement (Twiga)
2,100,000
19%

Tanga Cement (Simba)

1,200,000
11%
Mbeya (Bamburi)
700,000
6%

DSM Cement (Camel)
700,000
6%

Lake Cement (Nyati)
660,000
6%

Kisarawe Cement

300,000
3%

Fortune Cement
300,000
3%

Sungura Cement
300,000
3%

Moshi Cement


300,000
3%

Rufiji / Mtwara Cement
100,000
1%

Arusha Cement

100,000
1%

Chalinze Cement

ZERO

ZERO

Kwahiyo nilichokiona katika kuthibitisha kile alichoongea Mheshimiwa Waziri. Muunganiko hautaweza kutawala soko. Kuongeza asilimia 19 kwenye asilimia 11 kutafikia asilimia 30 tu. Hii imekuwa wazi kwangu sasa. Pia niliona mara nyingi sana Tanga na Twiga wakisaidia jamii mbalimbali nchini, huku viwanda vingine vikiwa havifanyi hivyo.

Nimeshawishika na kufurahishwa na serikali yetu na kazi kubwa wanayofanya ya kusaidia uchumi wa Tanzania.

Kila la kheri la Muunganiko wenu!

No comments