TBS WAITAKA JAMII KUZINGATIA MAELEKEZO YA UTUMIAJI WA CHAKULA , KUELEKEA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI JUNI , 7
Kaimu Meneja Kitengo cha Tathmini ya Vihatarishi vya chakula TBS, Dkt.Ashura Kilewela akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 25,2023 , katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 7 Juni kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni '' VIWANGO VYA CHAKULA HUOKOA MAISHA ".
KATIKA kuelekea Maadhimisho ya Chakula Salama Duniani Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeitaka Jamii kuzingatia kiwango kinachoelekeza kipimo cha chakula na ufungashaji na kuwasihi watumiaji wa vyakula kuzingatia maelekezo ya utumiaji wa chakula husika ambayo sana sana hupatikana katika vifungashio , hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Tathmini ya Vihatarishi vya Chakula Dkt. Ashura Kilewela wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya TBS Jijini Dar Es Salaam
AIDHA kuelekea Maadhimisho hayo TBS inawakumbusha wananchi kutumia chakula salama hasa katika uzingatiaji kwenye uandaaji kwa kutumia malighafi safi pamoja na utunzaji wa chakula.
No comments