TAASISI YA GREEN KIDS & YOUTH FOUNDATION YAJA NA MTOTO JITAMBUE
Mkurugenzi wa Taasisi ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet
Samson Mwazembe akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamano
la kuwainua wajasiriamali lenye kauli mbiu isemayo " Mjasiriamali Imara
chanzo cha familia bora" lililoandaliwa na taasisi hiyo ikishirikiana na
Benki ya CRDB pamoja na kuzindua mpango endelevu wa "MTOTO JITAMBUE".
Kutoka kushoto ni Katibu wa taasisi hiyo, Zawadi Thomas, Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Waitara, Diwani wa Vitimaalum
Jiji la Dar es Salaam,Beatrice Nyamisango na Ofisa Ustawi wa Jamii Ilala,
Joyce Maketa.
Katibu wa Taasisi ya Green Kids and Youth Foundation, Zawadi Thomas
akizungumza wakati wa kongamano la kuwainua wajasiriamali pamoja na kuzindua
mpango endelevu wa "MTOTO JITAMBUE" jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Waitara
akizungumza na wanawake wajasiriamali somo la thamani ya mwanamke katika jamii
wakati wa kongamano la kuwainua wajasiriamali lenye kauli mbiu isemayo
" Mjasiriamali Imara chanzo cha familia bora" lililoandaliwa na
taasisi hiyo ikishirikiana na Benki ya CRDB pamoja na kuzindua mpango endelevu
wa "MTOTO JITAMBUE" liliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa kituo cha Taaarifa na Maarifa Kitunda, Claudia Gabriel
akitoa somo la viashiria vya unyanyasaji wa kijinsia katika kongamano hilo.
Katibu wa Victorious Health Foundation, Edwin Rumboyo akitoa somo la
kukuza biashara katika kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Waitara
( wa pili kushoto ) akipokea risala ya Taasisi ya Green Kids and Youth
Foundation kwa Katibu wa Taasisi hiyo, Zawadi Thomas wakati wa wa kongamano la
kuwainua wajasiriamali pamoja na kuzindua mpango endelevu wa "MTOTO
JITAMBUE" lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
No comments