Breaking News

TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI MAONESHO YA 46 YA BIASHARA SABASABA YAJIKITA ZAIDI KWENYE KUTOA HUDUMA BORA

Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB),Joanitha Deogratias (wapili kushoto), akizungumza na baadhi ya watejawaliotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalim Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo.

Afisa Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Cornel Mlay (kulia), akizungumza na mmoja wa mteja  alietembelea banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki, kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere Barabara ya Kilwa. Katikati ni Afisa Uwendeshaji wa Benki hiyo Godbright Mlay.Afisa uwendeshaji wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Salha Singano (wapili kushoto) akitoa maelekezo kwa moja ya mteja alipotembelea Banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki, kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere Barabara ya Kilwa. kushoto ni Afisa wa kitengo cha ICT wa TCB Joseph BukuruMeneja Uhusiano wa wateja wakubwa wa Benki ya Biashara Tanzania TCB Shilla Senkoro  (kushoto), akizungumza na mteja kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki, kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Jk Nyerere Barabara ya Kilwa.

****************************************************

Benki ya Biashara Tanzania TCB imeshiriki maonesho ya 46 ya biashara Sabasaba ambapo benki hiyo imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa katika kuongeza matawi kila  mkoa na wilaya ili kusogeza huduma kwa wateja wake.

 

Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Meneja Mwandamizi Udara ya Mikopo wa benki hiyo Bi. Joanitha Deogratias alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.

 

“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wale wakubwa  pia mikopo kwa wastaafu kwaajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo za kiuchumi.

 

Joanitha alisema katika kuboresha huduma TCB imefanikiwa kutoa huduma za kibenki za kidigitali ambapo wateja wanaweza kufanya malipo mtandaoni kwa urahisi zaidi.

 

alisema benki hiyo imechukua hatua mbalimbali ili kutoa unafuu kwa wateja wake kutokana  hali ya kiuchumina ikiwemo kutoa unafuu wa riba.

 

“Sisi kama benki  ya Biashara Tanzania TCB tumefungua milango kwa wateja wetu wote waliokopa na ambao hawajakopa, tunataka kuwaendeleza wateja hasa kwa kusikiliza changamoto zao na tumeendelea  kufungua matawi Karibia nchi nzima, ” alisema.

 

Vilevile benki hiyo imechukua hatua yakuwakumbusha nakuwahimiza watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti.

 

Aliwahimiza watu wote waendelee kutembelea katika banda la Tanzania Commerci Bank ili kujionea huduma mbalimbali zinazopatikana katika benki hiyo.

No comments