TAMKO LA AFISA MADINI LINDI LAIBUA MAZITO , WACHIMBAJI WADOGO WAMUOMBA RAIS SAMIA
Na Mwandishi Wetu.
Vikundi hamsini vyenye wachimbaji wadogo zaidi ya 500 ambavyo vinaunda Chama Cha Wachimbaji Wadogo katika Mgodi wa Nditi maarufu kama " NTAKA HILL " wilayani Nachingwea Mkoani Lindi wamemuomba Rais Samia na Waziri wa Madini kuingilia kati simtofahamu inayoendelea hivi sasa baada ya wachimbaji hao kupokea barua inayowataka wahame na kusitisha Shughuli za Uchimbaji katika Mgodi huo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa RMO, Licha ya serikali kuonyesha kuwatambua na kuwaahidi kuwapa leseni kwa kipindi cha nyuma .
Akizungumza na Mwandishi Wetu Katibu wa Chama Cha Wachimbaji wadogo Katika Mgodi wa Nditi ( UVIWAMA ) Bwn. Castory Joseph Mtonga ameipongeza serikali kwa kutambua kuwa wapo katika mgodi huo na wanaendelea kujipatia Riziki huku wakiendelea kuchangia katika Shuguli mbalimbali za Kimaendeleo kama vile ujenzi wa Barabara km 16 kutoka Kata ya Mnelo mpaka kata ya Nditi, wamechangia fedha katika mfuko wa kijiji cha Nditi ambapo hadi sasa wamechangia Milioni 114 fedha ambazo zimetokana na Uchimbaji mdogo , kutoa ajira kwa zaidi ya Wachimba wadogo 500 ambao wanatambulika na wamesajiliwa serikalini , Michango mbalimbali wilayani , Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na Vyoo , Ujenzi wa Jengo la Akina mama kituo cha Afya na mambo Mengi ya kimaendeleo ambayo yamefanywa kutokana na fedha zinazotokana na Mgodi,
" Hakika tumechangia Mambo mengi ya kimaendeleo na wazawa wa eneo hili wanautegemea mgodi huu kujipatia kipato na hapo mwanzoni tuliaidiwa kutengewa kipande chetu kwa ajili ya wachimbaji wadogo lakini kwa sasa barua hii iliyokuja inaonyesha kutotutambua tena , Tunakuomba sana Mhe . Rais ahadi hiyo Iweze kutekelezwa maana Vijana na wananchi wengi wanyonge tunategemea mgodi huu ili tuweze kuendesha maisha yetu ya kila siku , Tafadhari tunaomba Mwekezaji huyu anayekuja atengewe eneo lake kama ambavyo serikali ilituahidi mwanzo kupitia Naibu Waziri wa Madini alipotutembelea mwaka jana, lakini pia mchakato wetu wa kupewa leseni uweze kukamilika haraka ".
Alimalizia Bwn. Castory
No comments