KAMPUNI YA YARA TANZANIA YAWATOA HOFU WAKULIMA UPATIKANAJI WA MBOLEA MSIMU WA KILIMO
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs 58,879,945.84 kwa mshindi wa kwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hapco Agrobusiness, Conrad Alex (katikati) baada ya kuibuka mshindi kwa kufanya mauzo mengi zaidi wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs 52,674,275.28 kwa mshindi wa pili, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nasa Kilimo, Nasa Mhina (wa pili kushoto) baada ya kuibuka mshindi kwa kufanya mauzo mengi zaidi wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs 27,321,514.80 kwa mshindi wa tatu, Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Mtewele General Traders, Deogratius Mtewele (wa pili kushoto) baada ya kuibuka mshindi kwa kufanya mauzo mengi zaidi wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (kushoto) akizungumza na washiriki wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulijadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Meneja wa Uagizaji na Uuzaji Nje wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Louis Kasera akizungumza na washiriki wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulijadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Obo Investment, Olais Oleseenga akiuliza swali wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulijadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili kwa msimu wa mwaka 2021/22.
Bwanashamba Mwandamizi Mstaafu wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Maulidi Mkima (kulia) akizungumza na wasambazaji wa kampuni hiyo wakati wakitembelea kiwandani hapo jijini Dar es Salaam juzi. Wasambazaji hao kutoka maeneo mbalimbali nchini walikuja kushiriki mkutano wa mwaka wa kujadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Kaimu Meneja Idara ya Uzalishaji wa kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Frank Lugoba (kushoto) akizungumza na wasambazaji wa kampuni hiyo wakati wakitembelea katika kiwanda cha Yara, jijini Dar es Salaam jana. Wasambazaji hao kutoka maeneo mbalimbali nchini walikuja kushiriki mkutano wa mwaka wa kujadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Wafanyakazi na wasambazaji wa kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, wakiselebuka kuhitimisha mkutano wao wa mwaka jijini Dar es Salaam jana.
No comments