Breaking News

YAS YALETA NGUVU MPYA KWA WAJASIRIAMALI KUPITIA KAMPENI YA "ANZIA ULIPO" KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2025

 Na Adery Masta.

Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba (DITF) yanaendelea kwa kasi jijini Dar es Salaam huku kampuni ya mawasiliano ya Yas ikitoa mchango mkubwa kwa wajasiriamali kupitia kampeni yake mpya ya "ANZIA ULIPO".


Kupitia kampeni hiyo, Yas imewawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati zaidi ya 20 kushiriki katika maonesho hayo kwa kuonyesha bidhaa na huduma zao kwa ajili ya kutanua wigo wa biashara zao na kukuza uchumi, jambo ambalo limechochea ari ya ujasiriamali na kuwapa hamasa ya kuamini kuwa ndoto zao zinaweza kuanza kutimia popote walipo.

"Kama si Yas, nisingekuwa hapa leo" – Mmoja wa washiriki, na Mjasiriamali Bw. Amos Boniface alieleza

 "Kwa kweli Yas wametufungua macho. Wametufundisha kuwa hatuhitaji kusubiri mtaji mkubwa kuanza, udhamini wao wa kutufikisha hapa tulipo , Maonesho haya yatafanya BIASHARA ZETU kujulikana Mkoani na hata  kimataifa. 

Kwa upande Mwingine Bi. Happynes Ruka amesema "Nimeweza kupata wateja wa kudumu kwenye maonesho haya. Kampeni hii imeniongezea uaminifu na exposure kubwa. Nawapongeza Yas kwa moyo huu wa kweli kusaidia vijana wa Tanzania."

Yas: Tunataka Watanzania Waamini Kuwa Inawezekana

Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Dar es Salaam Kusini, Bw. Robert Kasulwa, alisema:

 "Kupitia kampeni ya ANZIA ULIPO, tunalenga kuondoa hofu na kuleta ujasiri kwa wajasiriamali. Tunaamini kila mtu ana kitu cha kuanzia – iwe ni wazo, kipaji au bidhaa – na Yas ipo kuwapa jukwaa la kuonyesha uwezo huo."

Bw. Kasulwa aliongeza kuwa kampeni hiyo haitakomea kwenye maonesho ya Sabasaba pekee, bali ni mpango endelevu wa Yas kuwasogezea Watanzania fursa za kiuchumi kupitia mawasiliano na mitandao bora.


Yas imeleta pumzi mpya kwa vijana na Watanzania wanaojaribu kusimama na biashara ndogo ndogo. Kupitia "Anzia Ulipo", ujumbe umekuwa wazi – Huna haja ya kusubiri kesho kuanza kufanikisha ndoto zako. Anzia ulipo, sasa hivi.

No comments