Breaking News

YAS WAJA NA OFA YA SIMU ZA ZTE A35 NA A75 MAONESHO YA SABASABA

Na Adery Masta.

Dar es Salaam, Julai 5, 2025 – Katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara, kampuni ya Yas Tanzania kwa kushirikiana na ZTE Tanzania wamezindua rasmi simu janja mpya: ZTE A35 na A75, zikiwa na ofa maalum kwa wateja watakaotembelea banda lao katika viwanja vya Sabasaba.

Kupitia ofa hiyo, wateja wanapata:

Zawadi papo kwa papo ikiwa ni pamoja na:

 Fedha taslimu hadi milioni 1, Simu mpya, Earphones na bidhaa nyingine za thamani

Bi. Imelda Gerald, Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa Yas, amesema:

 “Tunawaletea bidhaa bora kwa bei rafiki, pamoja na motisha ya zawadi ili kila mmoja aweze kuanza safari yake ya kidijitali kwa ufanisi na furaha.”

Kwa mujibu wa ZTE, simu hizi zimeboreshwa kwa mahitaji ya sasa , Betri ya kudumu, Kamera zenye ubora, Hifadhi hadi GB 128, Muundo wa kisasa

Kwa wateja walio mbali na Sabasaba, ofa hii inapatikana pia katika maduka yote ya Yas nchini kwa kipindi chote cha mwezi wa Julai.








No comments