Breaking News

WAKULIMA WANUFAIKA NA SIMU JANJA ZA TIGO KWA BUKU TU

 KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo imekuja na njia ya kidigitali ya kumrahisishia mkulima kujifunza namna ya uzalishaji wa mazao bora kwa njia ya mtandao ambapo inatoa mkopo wa simu janja kwa wakulima ambao hutanguliza pesa kidogo ili waweze kumudu gharama za kupata simu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujifunza kilimo mtandaoni kupitia simu  za mkononi,Meneja mauzo na usambazaji wa Tigo mkoa wa Mbeya Ronald Richard amesema,kwa kutumia simu janja (Smart phone) mkulima anaweza kufanya kazi zake za kilimo kisasa zaidi na kuongeza uzalishaji.

“Tumeamua kuja na bidhaa hii kwa ajili katika maonyesho haya ya Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya kwa ajili ya wakulima na wananchi wote kwa ujumla ambayo inapatikana kwa kwa mkopo ambapo mtu anatanguliza pesa kidogo anachukua simu kisha anaendelea kulipia shilingi 1000 hadi 1500 mpaka mteja anapomaliza deni lake .”amesema Richard

Aidha amesema kuwa kabla ya kuanza kulipia malipo hayo ya kila siku mteja anatakiwa kutanguliza kiasi cha shilingi 70,000 hadi 90,000 kulingana na simu anayohitaji mteja.

“Njia hii ni rahisi kwa wananchi wengi hususani wakulima kuweza kumiliki simu janja ukizingatia simu huuzwa kwa bei ghali na hivyo wakulima wengi kushindwa kumudu gharama hizo.”amesisitiza

Hata hivyo kwa upande wake mkulima aliyezungumza na vyombo vya habari baada ya kununua bidhaa hiyo kutoka Tigo Abdul Said amesema,njia hiyo ni rahisi hususan kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kununua bidhaa hiyo kwa mkupuo.

“Tunaishukuru sana kampuni ya Tigo kwa kuja njia hii ambayo inaonekana kutujali sana wakulima hasa sisi wa chini ,kwani kwa kutumia simu hizi tunaweza kujifunza mambo mengi mtaandaoni yanayohusiana na kilimo na hivyo kutusaidia katika kuzalisha mazao bora na kwa tija.”amesema mkulima huyo


No comments