Breaking News

TBS WAENDELEA KUTOA ELIMU YA VIWANGO KWA UMMA KATIKA NGAZI YA WILAYA

                                 




Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi.  Gladnes Kaseka akitoa elimu ya Umuhimu wa Viwango kwa Wafanyabiashara wa Bidhaa za Chakula na Vipodozi Wilayani Malinyi ( kwa Nyakati tofauti tofauti ) pamoja na kuwaelezea utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora na kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi .
Afisa Usalama wa Chakula Mwandamizi TBS Bwn. Kaiza Kilango akitoa utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora na kusajili majengo ya Biashara kwa wajasiriamali wadogo wadogo kutoka Vijiji mbalimbali ndani ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro.

Na Mwandishi Wetu.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo Ndani ya Wilaya 63 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini. 

Akizungumza Leo Agosti 21, 2023 katika Wilaya Ya Malinyi mkoani Morogoro Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi.  Gladnes Kaseka amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.

" Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili  kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora na kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza kwahiyo Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia Wilaya 63 , Leo tupo hapa Malinyi vilevile tutaendelea na wilaya ya Ulanga,  Gairo na Mvomero katika Mkoa huu wa Morogoro ". amesema Bi.  Kaseka 

Nao Wajasiriamali kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya Ya Malinyi wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania Kwa Elimu waliyoamua kutoa kwa maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha.





No comments