Wafanyakazi Wa Absa Wasaidia Madawati Kwa Watoto Wenye Mahitaji
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utumishi na Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya (kushoto) akikabidhi madawati 37 yaliyowezeshwa kwa michango ya wafanyakazi wa benki hiyo kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Sezaria Kiwango ili kuwawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea. Madawati hayo yenye thamani ya sh milioni 10 yalikabidhiwa shuleni hapo, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Elimu Kata ya Gerezani, Mary Ruta na Ofisa Mauzo Absa, Jacqueline Asley.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utumishi na Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya akishikana mikono na baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi msaada wa madawati 37 yenye thamani ya sh milioni 10 yaliyopatikana kwa michango ya wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Kariakoo. madawati hayo yatawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya Absa Tanzania, George Binde (kushoto) akikabidhi madawati 37 yenye thamani ya sh milioni 10 yaliyopatikana kwa michango ya wafanyakazi wa benki hiyo Kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Sezaria Kiwango Katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Kariakoo, Dar es Salaam. Madawati hayo yatawawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (kulia) akisalimiana na Mwanafunzi.mwenye ualbino wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Mirfat Ibrahimu huku wenzake wakiangalia katika hafla ambayo wafanyakazi wa benki hiyo walikabidhi msaada wa madawati 37 yenye thamani ya sh milioni 10 shuleni hapo, Kariakoo, Dar es Salaam. Madawati hayo yatawawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea.
Wafanyakazi wa Benki ya Absa wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko baada kuwakabidhi msaada wa madawati 37 yenye thamni ya shilingi milioni 10 shuleni hapo, kariakoo, Dar es Salaam.
No comments