Absa yazindua Ripoti ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika
Naibu Katibu Mkuu (Sera), wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizindua ripoti ya Absa ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika, jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Absa, Simon Mponji, akitoa shukurani kwa Waziri wa Fedha pamoja na Naibu Katibu Mkuu kwa kukubali wito wa kufika katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam hiyo akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Absa kutoka ofisi ya Kanda, Jeff Gable akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Masoko ya Kifedha wa Absa Tanzania, Esther Maruma, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo jijini humo jana.
Naibu Katibu Mkuu (Sera), wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru (wa tatu kulia),na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Absa Tanzania, Simon Mponji (wa nne kushoto), wakionyesha kitabu chenye ripoti ya Absa ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika,mara baada ya kuzinduliwa kwake jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwa Mafuru ni Mkurugenzi wa Fedha wa Absa, Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Masoko ya Kifedha wa Absa Tanzania, Esther Maruma. Kushoto ni watoa mada, Anthony Kirui kutoka Absa Afrika, Abraham Byamungu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji (UNCDF), Charles Shirima kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) na Jeff Gable kutoka Absa Afrika.
Baadhi ya wageni waliolikwa katika hafla hiyo wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi naibu katibu mkuu sera wa wizara ya fedha jijini Dar es Salaam jana.
No comments