TIGO WASHIRIKI MKAKATI HUU MKUBWA KITAIFA
Mtandao namba moja nchini Tanzania kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Tigo , umeshiriki katika uzinduzi wa mkakati wa usajili wa uzazi kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Tigo kupitia matumizi ya teknolojia ya simu za mkononi imesaidia kurahisisha utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mkakati huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo CPA Innocent Rwetabura amesema kuwa
" Tigo tumechangia simu za mkononi zinazotumika katika usajili kwa mikoa yote 22, ambapo mpaka sasa tumefanikiwa kusajili zaidi ya watoto milioni 7.4.
Pia aliongezea kuwa Tabora tumechangia simu janja (smartphones) 542 zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 46. Simu hizi ndizo watakazotumia wasajili waliopatiwa mafunzo ili kuhakikisha watoto mkoani Tabora wanasajiliwa na taarifa zao zinatumwa kupitia mfumo wa SMS kwenda kwenye kanzidata (database) ya RITA. " alimalizia Kaimu mkurugenzi mkuu wa Tigo, CPA Innocent Rwetabura
No comments