MTANDAO WA WANAWAKE WAJASIRIAMALI TANZANIA ( TANEWE ) NA TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION WAFANYA MAKUBWA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited na Mlezi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Anita Gimero Waitara akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation pamoja na Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) jijini Dar es Salaam leo ambapo alikabidhi madaftari 500 pamoja na kula chakula cha mchana na watoto hao. Kushoto ni Diwani Kata ya Kitunda, Victor Vedasto.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet Samson Mwazembe (kulia) akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi hizo jijini Dar es Salaam leo ambapo walikabidhi madaftari 500 pamoja na kula chakula cha mchana na watoto hao. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Gimero Waitara na Diwani Kata ya Kitunda, Victor Vedasto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited na Mlezi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Anita Gimero Waitara (katikati) na Diwani Kata ya Kitunda, Victor Vedasto wakikabidhi madaftari kwa mmoja wa watoto wenye mahitaji maalum wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ), Vailet Samson Mwazembe.
Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) wakifanya zoezi la kukabidhi madaftari pamoja na kalamu wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo pamoja na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Shirika la Msaada wa Kisheria ( ILAP ), Salum Kindokomile akitoa elimu ya sheria kwa watoto wenye mahitaji maalum wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation pamoja na Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) wakigawa juisi kwa watoto wenye mahitaji maalum wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation pamoja na Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) jijini Dar es Salaam leo ambapo alikabidhi madaftari 500 pamoja na kula chakula cha mchana na watoto hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited na Mlezi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Anita Gimero Waitara ( aliyevaa koti jekundu), Diwani Kata ya Kitunda, Victor Vedasto pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) wakiserebuka na watoto wenye mahitaji maalum wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited na Mlezi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Anita Gimero Waitara ( aliyevaa koti jekundu) na Diwani Kata ya Kitunda, Victor Vedasto wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania ( TANEWE ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika jijini Dar es Salaam leo ambapo walikula chakula cha mchana na watoto wenye mahitaji maalum pamoja na kukabidhi madaftari 500.
No comments