Breaking News

TIGO GREEN FOR KILI , MITI 500 YAPANDWA ZAHANATI YA BOMANG'OMBE

 Kampuni inayoongoza nchini Tanzania kwa utoaji wa huduma za kidijitali, Tigo Tanzania, leo April 26, 2022  imepanda miche ya miti 250 kati ya 500 katika Zahanati ya Bomang'ombe wilayani Hai kama sehemu ya mradi wake unaoendelea wa Tigo Green for Kili, One Step One tree,  katika mkoa wa Kilimanjaro. 

Mradi wa Tigo Green for Kili, One Step One Tree ulizinduliwa mwishoni mwa Februari 2021, kwa lengo kuu la kuhifadhi theluji na mimea kuzunguka Mlima Kilimanjaro. Katika awamu ya kwanza, Tigo kwa kushirikiana na VOEWOFO na wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na ya umma ilikusanya zaidi ya miche 30,000 ya miti lakini ilifanikiwa kupanda zaidi ya miche 11,000 ya miti.

Akizungumza katika zoezi la upandaji wa miti hiyo katika Zahanati  ya Bomang'ombe Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe amewapongeza sana Tigo kwa kuendelea kutimiza kwa vitendo kampeni hii ya Tigo Green for Kili na kutoa wito kwa Jamii kutunza hii miti hiyo kwa maana ina thamani kubwa hasa katika kuendelea kutunza utheluji wa Mlima Kilimanjaro na Utalii kwa ujumla . Alimalizia Mbunge Mafuwe.

Kwa upande wake  Meneja wa Tigo Kilimanjaro Bwn. Aman Daraso amesema kuwa 

Katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani Tigo na wadau wao katika mradi huu VOEWOFO na wananchi wameamua  kuendelea kupanda miti hiyo ambapo kwa sasa wameshapanda miti Takribani Elfu 13 , alisema Bwn. Daraso.

Naye Mkurugenzi wa VOEWOFE Bi. Asfiwe James ameonesha kufurahishwa na Uongozi  wa Wilaya ya Hai na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla  kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika kuunga mkono kampeni hii ya Tigo Green for Kili Tangu kuzinduliwa kwake.


No comments