BENKI YA ABC YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 2 KUSAIDIA UJENZI WA CHOO CHA WAALIMU SHULE YA MSINGI MTAWALA MANISPAA YA MOROGORO.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga,(katikati), akikabidhi vifaa vya ujenzi wa Choo kwa Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya (wapili kutoka kulia), kulia Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akimkabidhi taarifa ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi , Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga akizungumza katika hafla hiyo.
Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati akisalimiana na waalimu waliojitokeza katika hafla hiyo.
Waalimu wa shule ya Msingi Mtawala.
BENKI ya ABC Kanda ya Morogoro, imekabidhi vitu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 2 katika kusaidia ujenzi wa Choo cha Waalimu katika Shule ya Msingi Mtawalaa Manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia kuondoa changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu hususani katika upande wa vyoo.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, imefanyika leo Aprili 20/2022 katika shule hiyo huku tukishuhudia Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro , Chausiku masegenya ,akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Masegenya, ameishukuru Benki ya ABC huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya Waalimu wengi kwa miaka mingi ijayo.
“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya ABC ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kuweka mazingira rafiki kwa waalimu ya kupata huduma ya choo , lakini pia kuwaondolea adha ya kutoka nje kwa ajili ya kufuata huduma ya choo" Amesema Masegenya.
Mwisho, Masegenya, ametoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya vyoo pamoja na mazingira ya kujifunzia katika shule za umma zilizopo Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.
Naye Diwani wa Viti Maalum anayetokana na Kata ya Mwembesongo, Mhe. Hadija Kibati, ameishukuru Benki ya ABC Kwa kuwaunga mkono kwenye sekta ya elimu kwa kuwapa vifaa hivyo ambayo yatasaidia kuondosha changamoto ya choo cha walimu shuleni hapo.
Kwa upande wa Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo, amesema kwamba utoaji wa misaada kwa jamii ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na kuona benki hiyo inachukulia kwa uzito sana suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu.
Kalinga,
amesema wametoa msaada huo ili kuunga mkono Serikali na juhudi za
wananchi na kurudisha kwao ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na hamasa ya
kutenegeneza miundombinu ya elimu kwa manufaa ya sasa na kizazi cha
baadae.
“Benki yetu inajivunia kuona Taifa linapiga hatua kubwa kwenye sekta ya elimu ambapo kupitia sera ya serikali elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi lakini pia ufaulu ambao maendeleo yake yanaakiisi hadi kiwango chetu cha uchumi ambapo mwaka jana nchi iliingia kwenye uchumi wa kati” Amesema Kalinga.
“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki yetu ya ABC, tumeguswa na changamoto ambayo iliwasilishwa kwetu , dhamira yetu kwa jamii ni kuona ni kuona tunaunga mkono na kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini na sio kwa Manispaa hii ya Morogoro pekee, hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo shuleni ili sasa Waalimu waweze kuwa na mahala rafiki kwa kutumia na kuacha kutoka eneo lao kwenda mbali na shule zao, ABC tutaendelea kushirikiana na Serikali kwa kadri tunavyoweza kuguswa na changamoto katika jamii ” Ameongeza Kalinga.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mtawala, Mwl. Godfrey Binagwa , ameishukuru Benki ya ABC kwa msaada huo ambao wameutoa ambao utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo za uhaba wa choo cha walimu.
Vifaa hivyo vya ujenzi ambayo walikabidhi benki hiyo ni Mifuko 50 ya saruji, mchanga Lori 1, Kokoto Lori 1, Mawe Lori 1, Milango 2 ya mbao, Fremu 2 za milango, Tofali za block 400 pamoja na Mabati 70.
No comments