Tanzania yatwaa taji la Cana kanda ya tatu kwa mara ya pili mfululizo
Na Mwandishi wetu
Tanzania imefanikiwa
kutetea ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu Afrika baada ya kuibuka katika nafasi ya
kwanza katika upande wa wanawake na wanaume.
Kwa mujibu wa
matokeo yaliyotangazwa juzi, timu ya Tanzania ilipata jumla ya
pointi 1,394 na kufanikiwa kuzishinda timu maarufu na kali katika mchezo huo,
Zambia ambayo ilipata pointi 968 na Kenya iliyomaliza ya tatu kwa pointi 957.
Uganda ambayo ndiyo
nchi ya kwanza kuandaa mashindano hayo, ilimaliza ya nne kwa kupata pointi 759
na kufuatiwa na Afrika Kusini iliyopata pointi 469 ma Sudani iliyopata oint 459
katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux,
Coca Cola, Label Promotions, Tanzania Sign Writers, Giraffe Ocean View, Print
Galore na Slipway Hotel.
Katika mashindano hayo
ya siku tatu, timu ya wanawake wa Tanzania ndiyo ilikuwa kali zaidi kutokana na
kuundwa na waogeleaji nyokta kama Sonia Tumiotto ambaye ndiye nahodha na
Natalie Sanford. Mbali ya hao kulikuwa na nyota wengine kama Maia Tumiotto
ambaye anakuja juu kwa kasi, Smriti Gorkan, Kayla Gouws, Amani
Doggart, Tara Behnsen, Emma Imhoff, Rania Karume , Chichi
Zengeni, Anjani Taylor, Anna Guild, Sanne Kleinveld , Angelica
Spence, na Tami Triller.
Kwa upande wa wanaume
, nyota alikuwa Marin De Villard pamoja na wakali wengine
kama Collins Saliboko, Joseph Sumari, Denis Mhini, Hilal
Hilal, Adil Bharmal, Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb
O'Sullivan, Khaleed Ladha, Matthew Guild , Chris Fitzpatrick, Harry
McIntosh, Dhashrrad Magesvaran na Joseph Sumari.
Kwa upande wa
timu ya Platnum, nayo ilionyesha kuwa kuna nyota wa baadaye wa Tanzania ambapo
timu ya wanawake iliindwa na Shivan Bhatt, Natalia, Charlotte
Sanford, Vanessa Dickson ), Rebecca Guild, Meredith Boo , Maria
Bachmann ), Kayla Temba na Maya Somaiya.
Kwa wanaume walikuwa
Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa,
Terry Tarimo, Aliasgar Chakera, Zeke Boos , Yuki Omari, Augustino Lucas
, Fallih Ahmed, Carter Helsby , Ian Lukaza na Emmanuel
Stenson.
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza aliwapongeza waogeleaji wa
Tanzania kwa kutwaa ubingwa huo huku akiahidi kutoa ushirikiano
mkubwa kwa chama cha kuogelea cha Tanzania (TSA).
Mwisho…
Waogeleaji wa timu ya
Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutetea vyema
ubingwa wa Cana kanda ya tatu.
Muogeaji nyota wa Tanzania, Sonia Tumiotto akipigania Taifa lake katika
mashindano ya Cana kanda ya tatu.
Collins Saliboko wa Tanzania akishindana katika mashindano ya Cana Kanda
ya Tatu Afrika
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi kombe nahodha
wa Tanzania, Sonia Tumiotto pamoja a Natalie Sanford mara baada ya kutwaa
ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu.
Makocha wa timu ya
Tanzania wakishangilia mara baada ya kutwaa ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu kwa
mchezo wa kuogelea.
Mashindano ya kuogelea
yana mashabiki wake, hapo watanzania wakishangilia kwa nguvu kuwapa hamasa
waogeleaji katika mashindano ya 'relay'.
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitoa nasaha zake wakati
wa mashindano ya kuogelea ya Cana Kanda ya tatu Afrika. Pembeni ni Mwenyekiti
waKamati ya maandalizi ya (TSA) Leena Kapadia na Rais wa Cana Kanda ya tatu Dk
Donald Rukare.
Muogeleaji wa
Tanzania, Denis Mhini akichumpa katika mashindano ya kuogelea ya Kanda ya ya
tatu ya Afrika.
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia)akibadilishana mawazo
na Mwenyekiti waKamati ya maandalizi ya (TSA) Leena Kapadia.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha kuogelea (TSA), Thauriya Diria na Katibu
Mkuu wake, Ramadhan Namkoveka wakiwa katika pozi la 'ushindi' mara baada ya
Tanzania kutetea ubingwa wa Kanda ya tatu wa Cana
Marin De Villard
(katikati) akipozi na waogeleaji wa Kenya mara baada ya kutangazwa kuwa
muogeleaji bora kwa upande wa wanaume.
Muogeaji nyota wa
Tanzania, Hilal Hilal akipozi na waogeaji wa Kenya mara baada ya kushinda
medali ya dhahabu.
No comments