Breaking News

Serikali kujenga mabwawa 10 ya kuogelea, Tanzania yaanza kwa vishindo

Serikali kujenga mabwawa 10 ya kuogelea, Tanzania yaanza kwa vishindo
Na Mwandishi wetu
Serikali imeahidi kujenga mabwawa 10 ya kisasa ya kuogelea kwa ajili ya kuendeleza mchezo  huo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika yanayoandelea kwenye bwawa la shule ya Kimataifa ya Heaven of Peace (Hopac).
Waziri Mwakyembe alisema kuwa wamefarijika sana na vipaji vya waogeleaji wa Tanzania katika mashindano  hayo ambayo yameshirikisha jumla ya nchi sita ikiwemo ya Tanzania. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Sudani, Afrika Kusini na Zambia.
“Nimesikitika sana kusikia kuwa kuna wawekezaji walikuja hapa kutaka kujenga bwawa la kuogelea kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huu na kukatishwa tamaa na baadhi ya watendaji wa wizara yangu,”
“Nawaahidi kulishughulikia suala hili kabla ya mwisho wa mwezi huu, nitakutana na Waziri wa Tamisemi na kuona ugumu upo wapi hasa kwa shule maarufu ya msingi ya Oysterbay ambayo ilikuwa iwe ya kwanza kujengewa  bwawa la kisasa la kuogelea,” alisema Waziri Mwakyembe.
Alisema kuwa malengo yake ni kuona mchezo wa kuogelea unafikia kiwango cha juu kabisa kwani amegundua nchi ina vipaji vingi, lakini wanashindwa kufikia kiwango cha juu kutokana na kukosa miundombinu ya kisasa.
Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka aliipongeza  serikali kwa ahadi hiyo ambacho ni kilio chao cha siku nyingi.
“Tumefarijika sana na ahadi za serikali, kama mnavyojua, tumekuwa tukiangaikia suala la kupata bwawa la kisasa la kuogelea miaka mingi, naamini mafanikio ya ahadi hiyo yataleta msisimko mpya kwa waogeleaji na wadau wake,” alisema Namkoveka.
Namkoveka pia aliwapongeza wachezaji wa Tanzania kwa kuanza kwa vishindi mashindano hayo na kutwaa medali 21 ambapo, nane ni za dhahabu. Waogeleaji, Sonia Tumiotto na Natalie Sanford kila mmoja alitwaa medali mbili za dhahabu katika mashindano hayo.
Waogeleaji wengine waliotwaa medali za dhahabu I Elia Imhoff, Emma Imhoff, Behnson Tara, Marin De Villard na timu ya relay kupitia kwa Collins Saliboko, Hilal Hilal, Sonia Tumiotto na Emma Imhoff.
Mwisho…

Muogeaji wa Tanzania kwa upande wa wanawake, Maia Tumiotto akishindana na wenzake katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza leo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini. Sonia alishinda katika mashindano hayo

Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania  wakijaindaa kuchupa katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza leo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania  wakijiandaa ku-dive  katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza leo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

 Waogeleaji kutoka nchi mbalimbali pamoja na Tanzania  waki-dive  katika mashindano ya  Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza leo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

Kocha wa timu ya Tanzania, Michael Livingstone akisimamia mazoezi ya timu ya Tanzania katika mashindano ya Cana Kanda  ya tatu yaliyoanza leo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Hopac ya jijini.

No comments