WAZIRI JAFO AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI TBS
.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo akishuhudia shughuli ya kula kiapo kwa Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo Septemba 05,2024,Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ifikapo mwezi Desemba,2024 kuwachukulia hatua za kisheria kwa wamiliki wa Viwanda na wazalishaji wa bomba (holepipes) wanaokiuka sheria za viwango vinavyowekwa na Shirika hilo ikiwemo kuteketeza bidhaa hizo na gharama za uteketezaji zitakuwa chini ya mmiliki wa bidhaa hizo.
Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya TBS Septemba 05,2024, kwenye Ukumbi wa Ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo, Jijini Dar es Salaam.
Dkt.Jafo ametoa maagizo hayo kutokana na malalamiko yaliyopo kwa wazalishaji hasa wa mabomba (holepipes) kutofuata viwango vilivyowekwa na shirika ambapo bomba moja linatakiwa kuwa na urefu wa mita 6 na unene wa milimita 1 na uwepo wa maelezo ya bidhaa(Mark)
Katika kuhakikisha kuwa Serikali inawalimda Wananchi wake Dkt.Jafo ameliagiza shirika hilo kushirikiana na Ofisi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kubaini wazalishaji wa vinywaji vikali ambavyo havifuati viwango cilivyowekwa na shirika hilo ambao ndio chanzo cha vifo vingi kwa Watanzania na kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa watumiaji wa bidhaa hizo nchini.
Aidha Dkt.Jafo amesema kwasasa mchakato wa kanuni ambao utakamilika hivi karibuni ambao utawataka wazalishaji wa bidhaa za chakula wanaongeza virutubisho ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto nchini hivyo TBS ina jukumu kubwa la kusimamia hilo
Vilevile Dkt.Jafo amelipongeza Shirika hilo kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kuiasa bodi hiyo mpya kuendelea na kazi nzuri zaidi ya pale walipoishia ili kuwa shirika bora kwa manufaa ya nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande amesema wapo tayari kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi wakiwemo wafanyabiashara na wenyeviwanda.
Amesema kwakuwa wajumbe wamekuwa wakihifahamu vizuri TBS, watahakikisha wanafanya yale ambayo watakuwa waagizwa katika kuhakikisha TBS inaendelea kufanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Septemba 05,2024,,Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande akitoa salamu za shukrani kwa Waziri wa Viwanda na Biashara wakati wa uzinduzi wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo Septemba 05,2024,,Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Ashura Katunzi akitoa salamu za ukaraibisho na shukrani katika uzinduzi wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo Septemba 05,2024,,Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hanifa Mohamed akizungumza na kutoa salamu wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Septemba 05,2024,,Dar es Salaam.
No comments