KIBOKO WATIKISA MAONESHO YA NANE NANE 2024 JIJINI DODOMA
Na Adery Masta.
Motisun Group Limited inayohusisha makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni namba moja nchini kwa Utengenezaji , Uuzaji na Usambazaji wa Bidhaa za Ujenzi ya KIBOKO , wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya Awamu ya sita kwa kazi kubwa ambayo amekua akiifanya ikiwemo kutoa nafasi na kuwatazama kwa jicho la kipekee wawekezaji wa ndani .
Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mkuu wa Makampuni ya Motisun Group Bwn. Erhard Mlyansi , Jana Agosti 08 , 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika kilele cha Maadhimisho na Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) Kitaifa Jijini Dodoma , ambapo kwa kutambua mchango wa Wakulima Motisun Group hasa Kampuni yake ya KIBOKO PAINTS wameshiriki maonesho hayo." Motisun Group ikiwa kama sehemu ya Makampuni yanayoigusa moja kwa moja Jamii na hasa wakulima kwa bidhaa zetu tunazozalisha katika Viwanda vyetu tumeona tufike kuwashirikisha Wakulima na Wananchi kwa ujumla ili wajionee bidhaa zetu bora tunazozizalisha hapahapa nchini , na katika siku hii muhimu ya NANE NANE tumeleta vifaa ambavyo vitawasaidia katika kuboresha Kilimo na Maisha yao Kiujumla , kwa sababu Maisha ni pamoja na nyumba na hapa tumekuja na bidhaa za Mashambani ikiwemo Mabomba , Matanki ya Kuhifadhia maji , Bati , Rangi n.k " amesema Bwn. Mlyansi
Aidha ameongezea kuwa Motisun Group kama kampuni ya wazawa wa hapa hapa Tanzania wameshiriki maonesho hayo kutaja sifa nzuri za Taifa letu kupitia Viwanda vyetu , kwa maana bidhaa za KIBOKO zinazolishwa hapahapa nchini suala ambalo linaongeza ajira kwa Watanzania na Ukuaji wa Uchumi wa nchi , lakini pia amewasihi Watanzania kununua bidhaa za KIBOKO ili kuviunga mkono Viwanda vya ndani na kukuza Uchumi wa Taifa letu.
No comments