TIGO PESA YASHEHEREKEA MAFANIKIO NA MAWAKALA WAKE
Na Mwandishi Wetu.
DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania imekutana na baadhi ya mawakala wake kutoka mikoa mbalimbali nchini Kwa lengo la kusheherekea mafanikio waliyoyapata katika mwaka 2023 na kueleza mikakati ya kuboresha huduma zao Kwa mwaka 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Afisa Mkuu wa Tigo Pesa , Bi. Angelika Pesha amesema mkutano huo unalenga kutoa elimu Kwa mawakala kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika kazi zao ikiwemo matapeli wa mitandaoni.
" Huu ni utaratibu wetu kama Tigo Pesa kila mwaka huwa tunatenga siku maalumu ya kukutana na mawakala wetu kutoka maeneo mbalimbali nchi nzima , na hawa ni baadhi kama ya mawakala zaidi ya laki mbili tulionao nao nchi nzima tumekutana nao ili tuweze kusheherekea nao lakini pia tuwape elimu ya jinsi ya kufanya miamala kwa usalama " alisema Bi . Pesha
Kwa upande wao Mawakala Said Mdee- Wakala wa Tigo Mbeya na Gladness Kazimoto- Wakala wa Tigo Dodoma wameipongeza kampuni ya Tigo kuwa kampuni ya Mawasiliano ya kwanza kufanya jambo kama ili la kuwakumbuka na kusheherekea mafanikio na mawakala wake , lakini kwa jinsi kampuni inavyowapambania mawakala wake wasiweze kuibiwa na matapeli wa fedha mitandaoni.
No comments