Breaking News

TIGO PESA KUTOA MKOPO WA HADI MILIONI 2 , WAJA NA NIVUSHE PLUS KWA KUSHIRIKIANA NA AZANIA BENKI

WAWEZA KUTAZAMA VIDEO HAPA
Na Mwandishi Wetu

Tarehe 27 Julai 2023. Kampuni ya inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tanzania, Tigo, inafuraha kutangaza uzinduzi wa bidhaa yake ya mikopo iliyoboreshwa kupitia Tigo Pesa kwa kushirikiana na Benki ya Azania. Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati wetu wa kuimarisha upatikanaji wa mikopo ya muda mfupi iliyopo na kukuza ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania ambayo kwa sasa imesajiliwa kwa asilimia 76%.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Pesa, Bi Angelica Pesha alisema, "Tunafuraha kuleta sokoni bidhaa ya mikopo iliyoboreshwa ya Nivushe Plus kwa kushirikiana na benki ya Azania kama sehemu ya mkakati wetu wa kuwawezesha wateja wengi zaidi kutumia huduma rasmi za kifedha kupitia simu zao za mkononi ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku kwa urahisi."

Huduma ya Nivushe Plus kama bidhaa iliyoboreshwa ya mkopo kuptia simu za mkononi ni huduma ya kwanza ya mkopo nchini Tanzania ambapo Tigo inatarajiwa kushirikiana na benki mbalimbali kutoa mikopo maalum kwa wateja wa Tigo Pesa wenye sifa. Huduma ya mkopo ya Nivushe Plus itawasaidia wateja wa Tigo Pesa kupata manufaa ya ziada ambayo ni pamoja na kupata kiasi kikubwa cha mkopo ikilinganishwa na vipimo vya awali vya mkopo. Kwa hiyo, wateja sasa wanaweza kukopa hadi TZS 2,000,000/-. hapo hapo kutegemeanan na pointi zao za ukopaji ambazo zinakokotolewa kutokana na matumizi yao ya huduma za Tigo Pesa.


Mkuu wa Kitengo cha Benki Kidijitali (Digital Banking) wa benki ya Azania, Vinesh Davda, akitoa maoni yake kuhusu ushirikiano na kampuni ya Tigo alisema, “Tunafuraha kushirikiana tena na Tigo Pesa katika jitihada za kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma za kifedha nchini Tanzania. Kwa kuunganisha utaalamu wetu wa kibenki na mtandao mkubwa wa huduma za kifedha kupitia simuz amkononi Tigo Pesa na ari ya uvumbuzi, tunatengeneza ushirikiano wenye nguvu ambao utaleta mapinduzi katika utoaji wa mikopo midogo midogo.”
Mafanikio ya Tigo Pesa kufikia kuwa mtoa huduma kamili wa huduma za kifedha yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubunifu na mtandao madhubuti kufuatia mpango unaoendelea wa kuboresha mtandao ambao umewezesha upatikanaji wa huduma za Tigo Pesa nchini kote.

Ili kuweza kupata huduma ya Nivushe Plus iliyoboreshwa, wateja wa Tigo Pesa wanaweza kupiga *150*01# au kutumia app ya Tigo Pesa na kuchagua Huduma za Kifedha.

No comments