TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MADAWATI 70 MKOANI TABORA
Mkuu wa wilaya ya Nzega Mh Naitapwaki Tukai akizungumza wakati wa hafla yakupokea msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo
Meneja wa Tanzania Commercia Bank Tawi la Nzega Shomari Shabani, (kushoto mwenyekoti jeusi), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Veronica Ng'waru kushoto kwake na Maofisa kutoka TCB pamoja na wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Benki ya TCB kukabidhi msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya kampeni Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo.
Tanzania Commercia Bank imetoa msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kusaidia Serikali kuboresha ubora wa elimu hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa benki ya TCB tawi la Nzega Bw. Shomari Shabani alisema msaada huo ni sehemu ya jitihada ambazo benki hiyo imekuwa ikifanya kusaidia jamii inayoizunguka.
Alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikijiweka mstari wa mbele kushirikiana na serikali kufanikisha mipango mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu, afya hapa nchini hatua inayopelekea kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa sekta zote ikiwemo ya benki pia.
“Mchango uliotolewa na Tanzania Commercia Bank wa kuchangia katika elimu unatokana na matumaini yetu kuwa bila kuwa na jamii iliyoelimika hata huduma za kibenki tunazozitoa zitadhoofika kutokana na ukweli kwamba biashara yetu hii inategemea sana mafanikio ya jamii inayotuzunguuka mafanikio ambayo tunaamini yataletwa na elimu,’’ alisema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa Wilaya ya Nzega Mh. Naitapwaki Tukai pamoja na kuishukuru Tanzania Commercia Bank kwa msaada huo alisema msaada huo umepatikana kwa wakati muafaka kwa kuwa shule hiyo ipo kwenye mkakati wa kutafuta madawati zaidi kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.
Alisema shule hiyo sasa bado inakabiliwa na uhaba wa madawati zaidi na hivyo kutoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuiga mfano kwa Tanzania.
No comments