BENKI YA MWANGA HAKIKA YAZINDUA TAWI JIPYA NA LA KISASA ARUSHA
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika Bank Eng. Ridhiwan Mringo (wa pili kushoto) wakifungua Kitambaa cha jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha,Wanaoshuhudia pembeni ni kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita .
Arusha. Aprili 28, 2023: Benki ya Mwanga Hakika (MHB) leo imezindua tawi jipya na la kisasa jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutanua mtandao wake wa huduma za kifedha nchi nzima.
Tawi hilo jipya lililopo katika jenga la Central Plaza, barabara ya Sokoine jirani na Clock tower jijini Arusha, linafanya idadi ya matawi ya benki hiyo kufikia saba. Matawi mengine yapo Dar es Salaam, Moshi, Dodoma, Mwanga na Same.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh alisema tawi hilo litaweza kurahisisha huduma kwa wateja wake na wakazi wa Arusha kwa ujumla.
“Tawi hili la hapa Arusha litarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kuwa lipo kati kati ya jiji. Tawi ni la kisasa na lina sehemu maalum kwa ajili ya wateja wakubwa, vifaa vya kisasa, huduma ya kubadilisha fedha nakadhalika. Hii yote ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma bora za kisasa na kwa urahisi,” alisema
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa tawi hilo limefunguliwa mahsusi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa fursa za kiuchumi zilizopo jijini Arusha zinaweza kuwafaidisha wakazi wa jiji hilo.
“Tawi linalozinduliwa leo ni sehemu ya mkakati wetu wa kujitanua na kuwafikia wateja wengi zaidi. Lengo letu ni kuwafikia wateja popote pale walipo lakini pia tukizingatia utoaji wa huduma bora za kifedha zinazoendana na mahitaji yao,” alifafanua.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba aliipongeza benki hiyo kwa kujikita katika kutoa huduma kwenye miradi ya miundo mbinu na kufanya kazi na wajasiriamali wadogo na wakati
“Napenda kuipongeza benki ya Mwanga Hakika kwa jitihada zake za kujitanua na hivyo kutoa fursa za wananchi wa kada mbali mbali kufikiwa na huduma za kifedha pamoja na kusaidia swekta mbali mbali ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu,” alsema
ENDS
No comments