Benki ya Absa yakabidhi msaada wa vifaa vya usafi Hospitali ya KCMC ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (wa nne kulia) akikabidhi vifaa vya kuhifadhia takataka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC, Prof. Gileard Masenga, vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Absa, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro Leo.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi, Pendo Abdallah akizungumza katika Kanisa la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kuhifadhia takataka vilivyotolewa na benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, hospitalini hapo, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga akizungumza katika Kanisa la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya kuhifadhia takataka vilivyotolewa na Absa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, hospitali hapo, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga, baadhi ya wafanyakazi wa Absa na watumishi wa Hospitali ya KCMC, wakipiga picha ya kumbukumbu katika hafla ambayo, Absa ilikabidhi msaada wa vifaa vya kuhifadhia takataka ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo mjini Moshi, Kilimanjaro Leo.
No comments