Tigo Zantel Zanzibar International Marathon Kuvutia Watalii Visiwani Zanzibar
Baadhi ya washiriki wa Tigo - Zantel International Marathon wakiwa tayari kuanza mbio mapema leo.
Viongozi Mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ( wa nne kutoka kushoto ) katika matembezi ya Km 5 Tigo Zantel Zanzibar International Marathon 2022 , Katika matembezi hayo wameambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Zantel CPA Innocent Rwetabura ( aliyevaa bukta nyeusi ).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Zantel CPA Innocent Rwetabura akimvisha medali Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman.
Viongozi Mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Zantel CPA Innocent Rwetabura katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa Tigo Zantel Zanzibar International Marathon 2022.
.......................................................................................................................................................
Na Mwandishi Wetu .
Leo Agosti 7 , 2022 yamefanyika mashindano ya mbio Visiwani Zanzibar Maarufu kama " Tigo Zantel Zanzibar International Marathon 2022 " mashindano yaliyoudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Rais wa Kwanza Zanzibar Mhe . Othman Masoud Othman
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa mbio hizo Mhe. Othman ameipongeza kampuni ya Tigo Zantel kwa udhamini wao wa mbio hizo kwa miaka mitatu na kuongezea kuwa hatua iyo itatoa hamasa kwa wakimbiaji kujitokeza zaidi na kupelekea kuzalisha vipaji vipya vitakavyoiwakilisha nchi kimataifa Zaidi .
" Binafsi niwapongeze Tigo Zantel maana kwa kudhamini mbio hizi kunatupa uhakika wa kuwepo kwa mbio hizi zenye hadhi ya kimataifa na ninaomba Wazanzibar watumia fursa hii kuonyesha bunifu zao mbalimbali kwa maana na hii ni sehemu mojawapo ya utalii " Alimalizia.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Zantel CPA Innocent Rwetabura ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusaidia kufanikisha tukio hili la kihistoria ndani ya visiwa ivyo
" Maamuzi yetu kudhamini mbio hizi yanadhiirisha nia yetu ya dhati ya kuwekeza katika jamhuri ya Muungamo wa Tanzania , maana tunaamini mbio hizi zinaibua fursa mbalimbali zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na kutangaza utalii wa nchi yetu .
Naomba niwakumbushe kuwa uwekezaji wetu katika mbio kama Tigo Half Marathon , Dodoma Marathon , Dam Dam Marathon na nyinginezo imechangia kuibua Vipaji mbalimbali vya riadha ambapo Wanariadha huanzia katika mbio hizi na kwenda kushiriki katika mbio kubwa zaidi za kimataifa .
Aidha niwapongeze waaandaaji wa mbio hizi pamoja na washiriki kwa kujitokeza kwa wingi hakika mmeacha historia ndani ya Visiwa hivi vya Zanzibar ". Alimalizia.
Nao kwa upande wao baadhi ya Washiriki wameipongeza Kampuni ya Tigo Zantel kwa kudhamini mbio hizi maana udhamini huu umezifanya zinoge zaidi na kuvutia watu wengi kushiriki , Aidha wamewaomba waandaaji kuongeza nafasi zaidi za ushindi walau kutoka tatu hadi kufikia tano , ili kutoa fursa zaidi kwa Watu kujitokeza zaidi kushiriki na kuonyesha ushindani wa kweli.
No comments