TIGO WAFUNGUA DUKA JIPYA MKOANI IRINGA
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI namba moja kwa utoaji wa huduma za Kidigitali nchini , Tigo Tanzania Leo Agosti 19 , 2022 imezindua duka jipya na la kisasa Mkoani Iringa Mjini_Mjini ambapo mgeni_rasmi_akiwa_ni_Mkuu_wa_Wilaya_ya_Iringa_Mhe. Mohamed_Hassan_Moyo.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Duka hilo Mkuu_wa_Wilaya_ya_Iringa_Mhe. Mohamed_Hassan_Moyo, ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa huduma nzuri na Bunifu mbalimbali walizonazo zenye lengo la kutoa huduma za kidigitali na kurahisisha maisha ya watanzania walio wengi, ikiwa ni sehemu ya adhima ya serikali ya kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na kunufaika na ulimwengu wa Kidigitali" WanaIringa_ni_wachapakazi_kufungua_naupanuzi_wa__duka_hili_kubwa_na_la_kisasa_lenye_hadhi_ya_kimataifa_kutawafanya_wana-iringa_kuendana na ulimwengu wa sasa, Tigo mmefanya jambo kubwa kwa wakazi wakazi hawa , maana sasa wananchi hawatahitaji kwenda mbali kufuata huduma na bidhaa za Tigo ambazo hapo awali zilikuwa zikipatikana katika maduka ya Tigo yaliyoko mbali na hapa , Duka hili litawasaidia wananchi wa eneo hili kuepuka usumbufu wa kusafiri kufuata huduma kwa maana nimeambiwa duka hili litatoa huduma kama uuzaji wa simu janja , Intaneti ya Nyumbani pamoja na ubadilishaji wa SIM, Tigo Pesa, huduma za usajili upya wa kibayometriki n.k hakika haya ni mapinduzi makubwa hongereni sana Tigo " . AlimaliziaNaye kwa upande wake Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kusini Bwn. Abbas Abdurahaman amesema “uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Tigo wa kuboresha utoaji wa huduma huku ikitimiza ahadi yake ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa bora na huduma kwa urahisi zaidi ndani ya mkoa wa Iringa ”.
Duka hili jipya litaweza kuhudumia hadi watu 300 kwa siku lakini pia lina eneo maalum la matumizi ambapo wateja wanaweza kupata fursa ya kufanya majaribio na kupata uzoefu wa bidhaa mbalimbali za Tigo kama vile simu za mkononi kabla ya kuzinunua.
Ahadi yetu kwa wateja ni kuwapa huduma za kibinafsi katika duka moja kwa mahitaji yao yote. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma zetu kunatokana na hitaji la wateja kufuata mtindo wa maisha wa kidijitali kote nchini. Mpango wetu ni kutoa masuluhisho jumuishi kama sehemu ya mkakati wetu wa kuendesha ushirikishwaji wa kidijitali katika ukanda huu” alimalizia Bwn. Abbas
No comments