Breaking News

Taasisi za Green Kids and Youth Foundation na Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) zafanya makubwa siku ya wanawake duniani 2022

Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe akizungumza na wanawake wajasiriamali somo la haki za mwanamke katika jamii wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani  yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo pamoja na  Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)  jijini Dar es Salaam jana. Maadhimisho hayo yalikusanya kata za Kitunda, Kivule na Mzinga pamoja na kuzindua mfumo wa maendeleo wa wanawake wa kata hizo.

Rais Mstaafu wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola ( katikati) akisindikizwa akiingia katika ukumbi wa Lukolo Inn wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation na Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)  jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Omto, Anna Haule.

Mabibi Maendeleo wa kata za Kitunda, Kivule na Mzinga wakiserebuka wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation na Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)  jijini Dar es Salaam jana. Maadhimisho hayo yalizindua mfumo wa maendeleo wa wanawake wa kata hizo utakao wezesha wajasiriamali kuwa na pensheni za uzeeni.

Rais Mstaafu wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola akizungumza na wanawake wajasiriamali somo la kujitambua mwanamke katika jamii wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation na Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)  jijini Dar es Salaam jana. Maadhimisho hayo yalikusanya kata za Kitunda, Kivule na Mzinga pamoja na kuzindua mfumo wa maendeleo wa wanawake wa kata hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Waitara akizungumza na wanawake wajasiriamali somo la thamani ya mwanamke katika jamii wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani  yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation na  Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)  jijini Dar es Salaam jana. Maadhimisho hayo yalikusanya kata za Kitunda, Kivule na Mzinga pamoja na kuzindua mfumo wa maendeleo wa wanawake wa kata hizo.

Mmiliki wa Ukumbi wa Lukolo Inn, Anita Lukolo akitoa somo la nidhamu ya uwekezaji katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Waitara akikata keki kuashiria uzinduzi wa mfumo wa maendeleo wa wanawake wa kata za Kitunda, Kivule na Mzinga utakao wawezesha wajasiriamali kuwa na pensheni za uzeeni wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation na Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO)  yaliyofanyika katika ukumbi wa Lukolo Inn  jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe ( kulia) na Mkurugenzi waTaasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule wakilishana keki kuashiria uzinduzi wa mfumo wa maendeleo wa wanawake wa kata za Kitunda, Kivule na Mzinga utakao wawezesha wajasiriamali kuwa na pensheni za uzeeni wakati wa wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi hizo jijini Dar es  Salaam jana.

Baadhi ya wanawake wajasiriamali wakihudhuria katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GS1, Fatma Kange ( katikati), Rais Mstaafu wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola na Mkurugenzi waTaasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule wakiongozana wakati wa maadhimisho hayo.

Mkurugenzi waTaasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza na wanawake wajasiriamali wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani  yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo pamoja na  Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gimero and Sons Limited, Anita Waitara (waliokaa katikati) akipiga picha ya pamoja na viongozi waalikwa pamoja kamati iliyiowezesha maadhimisho jhayo jijini Dar es Salaam jana.

No comments