NGAIZA FOUNDATION KUSHIRIKIANA NA DC ALBERT MSANDO KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI WILAYA YA MOROGORO
Wasema lengo ni kuhakikisha ifikapo 2025 suala la Migogoro Wilaya ya Morogoro linabaki historia. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. ALBERT MSANDO kwa kushirikiana na Taasisi ya NGAIZA FOUNDATION wanataraji kuendesha zoezi la utatuzi na usuluhishi wa Migogoro mbalimbali Wilayani humo ili kuiwezesha Serikali kupunguza changamoto hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi. ELIZABETH NGAIZA amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na miongoni mwa Mambo yatakayoshughulikiwa ni pamoja na Migogoro ya Ardhi, Mirathi, usuluhishi wa Migogoro ya ndoa pamoja na suala la matunzo ya mtoto. Aidha NGAIZA amesema Taasisi hiyo itatoa huduma hiyo bila malipo Chini ya Wataalamu wa masuala ya kisheria na utatuzi waliojitoa kuhakikisha kila Mwananchi atakaewasilisha kero na changamoto yake anasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi Jambo lake.
Hata hivyo Bi. NGAIZA amesema tayari Taasisi yake imefanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. ALBERT MSANDO ambae amepokea kwa mikono miwili Jambo hilo na ameahidi kushirikiana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Pamoja na hayo amesema anaamini kupitia Usuluhishi itasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zisizo na ulazima Mahakamani kwakuwa kipaombele Cha Taasisi hiyo ni upatanishi na pale inaposhindikana ndipo kesi zifikishwe ngazi ya Mahakama. Sanjari na hayo ametoa wito kwa Wananchi Wenye Migogoro kujitokeza kwa wingi kuwasilisha mashauri yao.
No comments