ABSA TANZANIA YAFUNGUATAWI JIPYA JIJINI DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya Absa Tanzania katika Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), jijini Dodoma jana. Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Oscar Mwamfwagasi, Ofisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Obedi Laiser na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge (katikati), na baadhi ya maofisa wa Benki ya Absa Tanzania kutoka kulia; Mkuu Idara ya Wateja Binafsi, Oscar Mwamfwagasi, Ofisa Fedha Mkuu, Obedi Laiser na Mkuu wa Mtandao wa Wateja, John Beja, wakishangilia mara baada ya mkuu wa mkoa kuzindua rasmi tawi jipya la benki hiyo katika Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), jijini Dodoma jana. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo na wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (wa pili kulia) katika hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini Dodoma jana. Wanaosikiliza kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Oscar Mwamfwagasi na Mkuu wa Mtandao wa Wateja, John Beja.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (katikati), pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo, wakikakata keki kuashiria uzinduzi wa tawi jipya a benki hiyo katika Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dodoma jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Binilith Mahenge (aliyekaa katikati), Ofisa Fedha Mkuu wa Absa Tanzania, Obedi Laiser (kushoto kwake), Mkuu wa Wteja Binafsi, Oscar Mwamfwagasi (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo mjini Dodoma jana.
No comments