Tamko la Nabii Suguye kwa Vijana
Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar es Salaam akiwahubiria waumini wa kanisa hilo (hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Waumini wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kanisani hapo wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Mmoja wa waumini wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, jijini Dar es Salaam, Msanii wa Maigizo nchini Jennifer Kyaka maarufu Odma akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kanisani hapo wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Mmoja wa wanenaji waliopata nafasi ya kuhubiri kanisani hapo Askofu Mkuu wa kanisa la CAG, Mtume Danstan Haule Maboya akiwahubiria waumini wa kanisa hilo (hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Mkewe Mwinjilisti Mkuu Anna Suguye kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Na Mwandishi wetu,
Nabii wa Kanisa la WRM lenye makao yake makuu Kivule Matembele ya Pili, Nicolaus Paul Suguye amewashangaa vijana wengi siku hizi kutumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kutuma na kutafuta picha zisizofaa na mijadala isiyo tija katika maisha yao.
Nabii Suguye ni mwanzilishi na mbeba maono wa huduma ya upatanisho ya WRM ameyasema hayo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo ambayo ilianza rasmi tarehe 14 februari, 2007 hapo hapo Kivule Matembele ya Pili.
“Biblia inasema…..mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo….. wa unasema mimi hapa sasa hivi nina nguvu, naweza nikafanya chochote, ndio muda sahihi Mungu anataka ukamtumikie”, alisema Nabii Suguye.
Suguye aliongeza kwa kusema “Wito wangu kwa vijana waache maovu wamkimbilie Mungu, kwake yeye kuna kila kitu, anaweza kuyasamehe makosa yao na kuwabariki badala ya kutumia muda wao mwingi kwenye mitandao na kuchafua watu, kuandika lugha zisizofaa mitandaoni, na kutazama picha zisizofaa zitakazoharibu mustakabali wa maisha yao ya baadaye.”
“Ikumbukwe nguvu kazi ya Taifa iko kwa vijana, hivyo tukiwa na vijana wenye hofu ya Mungu, Mungu atajivunia na taifa pia litajivunia” alimalizia Suguye.
No comments