Breaking News

RC MAKONDA, AWAKABIDHI WALIMU VIJIBWENI, OFISI YENYE HADHI YA KIMATAIFA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (wapilikushoto), akipokea mfano wa funguo  kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRJE (EAST AFRICA)  ya nchini China Bai Hao Chen (wapili kulia), wakati wa hafla  ya kukabidhi majengo ya Ofisi za Walimu wa Shule ya Msingi Vijibweni, Kigamboni leo. wengine (kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafili Makamu Mwenyekiti Kamati ya Ujenzi Ofisi hizo  ACP Solomon  Urio kutoka Jeshi la Magereza, wengine ni Afisa Elimu Mkoa Hamisi Lissu, na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kushoto), akishikana mikono  na Meneja wa Tawi la CRJE (EAST AFRICA)  ya nchini China Bai Hao Chen, wakati wa hafla  ya kukabidhi majengo ya Ofisi za Walimu wa Shule ya Msingi Vijibweni, Kigamboni leo.

Mkuu wa Mkoa akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Hii ndio Ofisi ya kisasa kabisaa ya walimu Shule ya Msingi vijibweni Katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amekabidhi jengo la Ofisi za walimu Katika Shule ya Msingi VIJIBWENI Katika Wilaya ya kigamboni ambapo hapo awali walimu walikosa ofisi kwa ajili ya kufanya kazi yao kwa ufanisi.

Awali walimu katika Shule hiyo walikuwa wakikaa nje,na  kufanya kazi chini ya Miti,kwenye vikorido,kwenye madawati Pamoja na  kujisaidia kwa majirani kutokana na ukosefu wa ofisi Pamoja na choo kwa ajili ya walimu hao, kutokana na adha hiyo RC Makonda amekadhi jengo la Ofisi hizo zilizojengwa na Kampuni ya CRJE.

Ofisi hiyo ya kisasa  ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 200 ambapo ndani yake ina ukumbi mikutano, Ofisi ya mwalimu mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi,ofisi ya walimu wote, Chumba cha kuhifadhi mitihani, stoo, sehemu ya mapokezi, chumba cha kubadilishia nguo, vyoo vya kisasa na bafu huku ikiwa imefungwa viyoyozi (AC) ili kuhakikisha walimu wanafanya kazi kwa uhuru.

Akizindua ofisi hizo  amesema dhamira yake ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira bora ipo palepale kwakuwa anatambua thamani ya mwalimu ni kubwa kwenye jamii hivyo wanastahili kupewa heshima.

Aidha ameishukuru Kampuni ya CRJE East Afrika ya nchini China iliyoamua kumuunga mkono kwa kujenga ofisi mbili za walimu kwa lengo la kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira mazuri.

Kwa upande wao walimu wa Shule ya Vijibweni kwanza wamemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea ofisi hiyo ya kisasa kwakuwa awali walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo chini ya miti na wamekuwa wakitumia choo kimoja na wanafunzi na wakati mwingine kujisaidia kwa majirani wenu.

No comments