Breaking News

Benki ya NBC na Asasi ya Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) zaingia makubaliano kusaidia Kilimo Biashara nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay, makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa  sekta ya kilimo biashara nchini. NBC pia ilipokea mfano wa hundi ya Dola 1,000,000 kutoka PASS zitakazotumika kama dhamana katika mikopo ya kilimo itakayotolewa na benki hiyo. Hafla ilifanyika jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akisaini hati za makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay, makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa  sekta ya kilimo biashara nchini. NBC pia ilipokea mfano wa hundi ya Dola 1,000,000 kutoka PASS zitakazotumika kama dhamana katika mikopo ya kilimo itakayotolewa na benki hiyo. Hafla ilifanyika jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi wa Dola 1,000,000 kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa  sekta ya kilimo biashara nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto, walioketi) na Mkurugemzi Mtendaji wa PASS, Nicomed Bohay (kushoto kwake), wakipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na watumishi wa taasisi hizo mbili mara baada ya kumalizika kwa tuki hiyo mjini Arusha leo.

SEKTA ya kilimo na ufugaji  nchini kupitia Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya  Kilimo (PASS) na Benki ya NBC Tanzania wameingia katika ushirikiano wa kuwawezesha wakulima nchini kupata mikopo ili kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta hiyo.

Akiongea kwenye utiaji wa saini makubaliano ya ushirikiano huo wa miaka mitano,  kati ya PASS na NBC jijini Arusha leo,  Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi amesema kuwa ushirikiano huo utawezesha benki hiyo kutekeleza mipangokazi yao ya kuongeza mnyororo wa thamani katika kilimo biashara.

Ameeleza kuwa ushirikiano huo kati ya taasisi hizo mbili utawezesha wakulima wafugaji nchini kupata mafunzo bora yenye tija ya kuongeza mapato au mavuno, uandaaji wa maandiko ya kibiashara na uwekezaji kwenye kilimo,kupata huduma za kilimo kwa makundi,kujengewa uwezo wa kuendesha biashara kwa faida na dhamana ya mikopo hadi asilimia 60%.

Amesema kuwa hayo yote yanalenga kumwezesha mkulima na mfugaji kutoka pale alipo na kuendelea kukua ili aweze kutoa mchango wake katika kujenga uchumi imara wa nchi yetu na huduma hizi zinapatikana katika matawi yoteya NBC nchi nzima.

“Niwaombe wadau wa kilimo na mifugo nchini kuchangamkia fursa hii kwa kutembelea katika matawi yetu na makubaliano haya kati yetu na PASS ni kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa na yatakuwa bora na yenye manufaa makubwa kwa wadau wa sekta ya kilimo kwa siku za usoni”alisisitiza Sabi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Asasi ya kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay ameeleza kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia wateja katika kuandaa miradi bora ya uwekezaji ambayo inaweza kupatia faida kubwa na kuwezesha upatikanaji wa huduma za fedha kwa ajili ya ufadhili wa miradi kupitia udhamini wa mikopo kwa kushirikiana na benki za kibiashara.

Amesema kuwa wameshaingia makubaliano na benki za kibiashara 16 nchini na makubaliano hayo na benki ya NBC taasisi yao imetoa dola za kimarekani million 1 kwa ajili ya udhamini wa mikopo ambayo itatolewa kwa wakulima na wafugaji kupitia benki ya NBC.

“PASS imeendelea kuwa shirika la mfano, jumla ya wajasiriamali wa kilimo 929,172 wamefaidika na mikopo iliyodhaminiwa na PASS inayofikia shilingi bilioni 712 kati ya mwaka 2000 na 2018,” alisema.




Pamoja na hayo Mkurugenzi wa PASS aliongeza kuwa, mwaka 2019 ni mwaka wa pili wa mpango mkakati wao wa miaka mitano (2018-20220 wakilenga kuutengeneza ajira 700,000 kupitia sekta ya kilimo wakitarajia familia zipatazo 235,253 kunufuaika kupitia mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 210.6.

No comments