WAITARA AWATAKA VIONGOZI WA MITAA KUWASHIRIKISHA WANANCHI MIRADI INAYOINGIA MITAANI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara (kushoto) akisalimiana na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala pia Diwani wa
Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto baada ya kuwasili kata ya
Ukonga na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo wakati wa ziara yake ya kutoa
shukrani baada ya kuchaguliwa Ubunge kwa mara ya pili pamoja na kutoa mirejesho ya kero ambazo
zinasumbua katika kata hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga , Mwita Waitara
akizungumza na wakazi wa kata ya Ukonga na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam
leo wakati wa Ziara yake ya kutoa shukrani baada ya kumchagua kuwa Mbunge wa
jimbo hilo kwa mara ya pili pamoja na kupata uteuzi wa Unaibu Waziri.Huu ni mwendelezo wa Waitara kutembelea kata zilizopo Jimbo
hilo kutoa Shukrani vilevile kutokana na kipindi hiki cha kuandikisha Watoto
kuingia Darasa la Kwanza amekemea suala la Michango ya manyanyaso mashuleni.Na
amehusia kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa kuwashirikisha wananchi miradi
inayoingia katika mitaa yao hivyo basi itasaidia kuondoa maneno maneno ya
kuonekana Viongozi wa juu hawafanyi kazi zao kiuwadilifu.
Naibu Meya wa Manispaa ya
Ilala pia Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto) akizungumza katika hafla
hiyo.
No comments