MAHAFALI YA SHULE YA MSINGI KITUNDA YALETA NEEMA
Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa wa Amani kata ya Kipunguni, Daniel Malagashimba (wapili kulia)
akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitunda (hawapo
pichani) wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba
iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.Mwisho kulia ni Mkuu wa
Shule hiyo Shani Mbunda, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Shule, Julius Kamugisha na Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kitunda,
Mwanahawa Zinga.Vilevile Mheshimiwa Malagashimba aliahidi kuchangia
Mifuko ya Simenti 20 kwa niaba ya Diwani wa Kata ya Kipunguni, Mohamedi Msophe
mifuko 10 alitoa wakati wa hafla hiyo na mingine 10 ameahidi kuikabidhi siku
zijazo kutokana na mwamko huo wa Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
kata ya Kipunguni umehamasisha baadhi ya wazazi wa shule ya msingi Kitunda nao
kuchangia mifuko ya Simenti kwa ajili ya ukarabati wa mindombinu ya Shule hiyo.
Mkuu wa Shule ya
Msingi Kitunda, Shani Mbunda (Kulia) akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi
(hawapo pichani) katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la
saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.Wapili kulia ni Mwenyekiti
wa Serikali ya mtaa wa Amani kata ya Kipunguni, Daniel Malagashimba, Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Shule, Julius Kamugisha na Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Kitunda, Mwanahawa Zinga.
Mwenyekiti wa Serikali ya
mtaa wa Amani kata ya Kipunguni, Daniel Malagashimba (kulia) akimlisha keki Mzazi
wa Shule ya Msingi Kitunda kuashiria shukrani ya kusaidia kuchangia mfuko mmoja
wa Simenti kwa ajili ya ukarabati wa mindombinu ya shule hiyo wakati wa hafla
ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo
jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mkuu wa Shule ya Msingi Kitunda, Shani
Mbunda.
Baadhi ya wahitimu wa
Darasa la saba pamoja na wanafunzi wa madarasa ya chini wakisikiliza kwa makini mada zinazotolewa na walimu wao katika
sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika shuleni hapo jijini
Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa wa Amani kata ya Kipunguni, Daniel Malagashimba (wapili kulia)
akikabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya msingi kwa mmoja wa Wanafunzi wa shule
ya Msingi Kitunda wakati wa sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa darasa
la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Julius Kamugisha na Kaimu Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kitunda, Mwanahawa Zinga.
No comments