Rais Magufuli aombwa kuwanyonga washtakiwa wa mauaji ya Albino
Na James Timber, Mwanza
Mwenyekiti wa Watu wenye Ulemavu Ngozi (Ualbino) jijini Mwanza Alfred Kapole, amemuomba Rais Dk.John Magufuli kuwanyonga watu wanaoshikiliwa kwa makosa ya mauaji ya watu wenye ualbino.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Muungwana Blog amesema kuwa, wale waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe mpaka kufa ili haki itendeke sawa na iwe fundisho kwa wengine ambao wanampango wa kufanya vitendo hivyo waogope kutokana na makali ya sheria.
"Katiba yetu inatuongoza lakini cha ajabu hatujaona lolote kuhusu kuwanyonga watu wanaoua wenzao kwa makusudi tunaumia kuona mtu aliyeua kuendelea kula chakula cha nchi hii ambacho sisi wahanga ndio tunakatwa kodi inayochangia ununuzi wa chakula hicho," alisema Kapole.
Kapole amesema hofu imetanda kwa walemavu wa ngozi wanaishi kwa wasiwasi tangu itokee tukio la mtoto mwenye ualbino katika Wilaya ya Tarime aliponyolewa nywele kisha kukatwa kucha.
Pia amesema kuwa baada ya Sikukuu ya Pasaka alihisi watu wabaya waliofika nyumbani kwake wilayani nyakati za usiku kilichomsadia ni kupiga yowe ambapo watu hao walimkimbilia kusikojulikana.
Aidha ameiomba jamii inayowazunguka kuwa karibu na watu wenye ualbino, kwani itapunguza changamoto hizo wanazokumbana nazo mara kwa mara.
No comments