Breaking News

YAS WAFUNGUA DUKA JIPYA DAR VILLAGE MALL DAR ES SALAAM.

Kampuni ya mawasiliano ya Yas kwa kushirikiana na Yas Mixx leo Oktoba 10, 2025 imezindua duka jipya Dar Village Mall, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kusogeza huduma karibu zaidi na wateja pamoja na kuunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, inayoadhimishwa duniani kote, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mission Possible”—ikielezea kwa kina dhamira ya kampuni hiyo kuwa mshirika wa kweli wa Watanzania katika safari yao ya mafanikio ya kidijitali.


Kupitia duka hilo jipya, Yas inalenga kutoa huduma za kisasa na bora zaidi kwa wateja wake, zikiwemo msaada wa papo kwa papo, ushauri wa kitaalamu, na nafasi ya kujionea kwa vitendo teknolojia ya 4G na 5G inavyofanya kazi katika maisha ya kila siku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mixx, Bw. Anold Ngarashi alisema kampuni hiyo inalenga kuchochea fikra tunduizi kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na watumiaji wa huduma za kidijitali, ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Yas na Mixx, Bi Mwangaza Matotola alisema wiki hii ni fursa muhimu ya kuimarisha mahusiano na wateja, na kuwasaidia kuzifikia fursa zinazotolewa na ulimwengu wa kidijitali kwa karibu zaidi.






No comments