Breaking News

DIT KUWAPIGA MSASA WATUMISHI , UVUJISHAJI WA TAARIFA ZA UMMA

 Na Mwandishi Wetu.

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayoanza leo jumatatu Juni 16 hadi Juni 23, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imejipanga kutoa semina elekezi kwa watumishi wake juu ya matumizi sahihi ya tehema ili kuboresha utolewaji wa huduma kwa wanafunzi, watu kutoka nje ya Taasisi pamoja na watumishi wa Taasisi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa DIT, Mipango, Fedha na utawala, Bwana Daudi Simbeye akimuwakilisha Mkuu wa DIT Prof. Preksedis Michael Ndomba katika ufunguzi wa wiki ya Utumishi wa Umma katika taaisi hiyo.


"Lengo la kuadhimisha wiki hii ni kujadili, kupeana uwelewa kwa watumishi wetu ili kuboresha huduma zetu kwa wateja wetu" Amesema Bw. Simbeye.


Amesema katika kutekeleza jukumu hilo watumishi wanapaswa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zinazoongoza watumishi wa umma katika kuboresha huduma.


"Taasisi yetu (DIT) imeweka juhudi zaidi katika kuingia matumizi ya Kidigitali lakini juhudi hizo wakati mwingine tunakumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la maadili katika kutoa huduma. Kwa maana inatuwekea wakati Mwingine kuvujisha taarifa au siri kwa wale wasio husika" 




Ameongezea kuwa ili kukabili suala la kukosekana kwa maadili kwa watumishi wa Umma, Taasisi imealika wataalamu kutoka nje ya Taasisi hiyo, ambao watafundisha mada mbalimbali katika utumishi wa Umma ikiwa ni kujifunza hasa matumizi ya kidigitali , maadili katika matumizi ya kidigitali na sheria za kiutumishi.

No comments