YAS YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUCHANGAMKIA FURSA ZA HUDUMA JUMUISHI ZA KIFEDHA
Kaimu Mkurugenzi wa Yas – Kanda ya Kaskazini, Bw. Daniel Mainoya (wa pili kushoto), akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Mkude (wa pili kulia), wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa chapa za Yas na Mixx by Yas jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano – Mixx by Yas, Justine Lawena, na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa – Yas Business, Anatory Lelo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa chapa za Yas na Mixx by Yas jijini Arusha jana.Alitoa wito kwa wakazi wa Arusha kutumia kikamilifu huduma hizo ambazo zimebuniwa kujibu mahitaji ya wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini.
Kaimu Mkurugenzi wa Yas – Kanda ya Kaskazini, Bw. Daniel Mainoya akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa chapa za Yas na Mixx by Yas jijini Arusha jana.YAS inaleta mapinduzi ya huduma za kifedha kidigitali, hususan kwa vijana, ili kuboresha maisha yao na kuongeza fursa za kiuchumi.
Baadhi ya Wadau wa Kampuni ya Yas wakihudhuria wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Mkude na Kaimu Mkurugenzi wa Yas – Kanda ya Kaskazini, Bw. Daniel Mainoya (kulia kwake) wakipiga picha ya pamoja baada ya kuzindua rasmi chapa za Yas na Mixx by Yas jijini Arusha jana.Kwa ujumla, YAS imejikita katika kuhakikisha kuwa huduma zake zinapatikana kwa urahisi, usalama na kwa gharama nafuu, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono ajenda ya taifa ya kujumuisha wananchi wote katika huduma za kifedha.
Post Comment
No comments