Breaking News

TIGO WASHIRIKI MBIO ZA MBEYA TULIA MARATHON 2024

 Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Tigo leo Mei 11, 2024 imeshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024 zilizoandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Tulia Trust. Mbio hizo zilianzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024.

Mbali na Kampuni ya Tigo Baadhi ya viongozi wa Kiserikali walioshiriki mbio hizo ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Kassim Majaliwa, Mke wake Mary Majaliwa, Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, Wakuu wa Mikoa ya Njombe na Mbeya, Wabunge na Viongozi wa Vyama vya Siasa.











No comments