Breaking News

MY LEGACY WAHIMIZA VIJANA KUTUMIA UJUZI WALIONAO KUISAIDIA JAMII

Na Mwandishi Wetu.

MRATIBU wa Taasisi  isiyo kuwa ya  Kiserikali la My Legacy Amina Ally  amewaasa vijana kujitolea na kuwa chachu wa kutafuta Suluhu na chagamoto zilizopo katika jamii zao .

 Amina  ametoa wito huo jijini Dar es salaam leo Februari 9 , wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi zinazofanywa na Shirika hilo, amesema Shirika  hilo limekuwa likifanya kazi katika jamii ili  kutokomeza umasikini na kuishi maisha yenye staha.

Akitaja  maeneo ambayo Shirika hilo limekuwa likifanya kazi ya uwezeshaji wa wanawake, vijana kiuchumi na Uongozi shirikishi pamoja utetezi wa haki za wanawake na watoto.

"Lengo kuu la Shirika letu ni kufanya  kazi na makundi mbalimbali katika kuhakikisha jamii zinapata ujuzi wa kuweza kutatua chagamoto mbalimbali walizonazo katika jamii zao,"amesema.

Mratibu huyo programu aliendelea kueleza kuwa kupitia programu  ya uongozi shirikishi ( kujitolea) wamekuwa wakifanya kazi na Makundi mbalimbali ikiwemo watoto hasa waliopo shule kupitia klabu zao.

Amesema pia taasisi hiyo ya My Legacy imetoa elimu ya ujuzi kwa wanafunzi kupitia klabu zao za shule, kuhakikisha jamii zinaishi maisha ya staha  na zinatokomeza umaskini.

-Ujuzi wanaofundishwa ni kutengeneza batiki, sabuni, kupanda miti ya matunda, miti ya kivuli, bustani za mboga mboga na kutengeneza sodo.

Kundi lingine ni  vikundi katika jamii ikiwemo vya watu wenye ulemavu, pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka sekta ikiwemo usimamizi wa miradi.

Hata hivyo amesema  Taasisi  hiyo imekuwa ikifanya kazi na wanafunzi waliopo vyuoni na waliomaliza kutokana na wengi wao wamekuwa hawana ujuzi unaohitaji kwenda kujipatia ajira.

"Tumekuwa tukipokea vijana kutoka  vyuoni waliopo na waliomaliza wengi wanapotoka chuo mara nyingi wamekuwa hawana ujuzi unaohitaji kwenda kujipatia ajira  hivyo tumekuwa tukiwapokea na kufanya nao kazi kwa kuwapatia ujuzi ili pale watakapo pata kazi sehemu nyingine waweze kutumia ujuzi walioupata kwa kuleta maendeleo,"amesema Amina

Aidha amesema Taasisi hiyo inaamini  katika kufanya kazi kwa kujitolea, kwa pamoja kwa kushirikiana kunaweza kuleta mabadiliko hasa katika jamii  na kuondoa chagamoto zinazoikabili ikiwemo masuala ya usafi, haki za wanawake na watoto.

"Kupitia rasilimali watu kwa pamoja tunaweza kusaidia kuja na bunifu ambazo zitasaidia kutengeneza programu na Suluhu katika jamii, "alisisitiza.

Kwa upande wa wanufaika wa mafunzo  kutoka Taasisi hiyo wameipongeza kwa kuwapatia mafunzo ambayo yameweza kuleta mabadiliko kwao na  katika jamii anayoishi.

Ally Yusuph, Katibu wa  Taasisi ya Green beach amesema Shirika hilo limewezesha kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa katika kikundi chao ambacho  kimejikita katika kufanya kazi za kujitolea.

No comments