Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi yazinduliwa jijini Dar
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula (wa pili kushoto) na Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Rukia Yazid, wakizindua nembo kuashiria uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022 jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022. Wengine ni viongozi wa TPSF na wawakilishi wa makampuni wadhamini.
Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Rukia Yazid (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula, viongozi wa TPSF na wawakilishi wa makampuni wadhamini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula, akipokea mfano wa hundi ya shs 58,300,000 kutoka kwa Mkuu Uendeshaji wa Kundi la Makampuni ya Bravo, Evarist Maganga (wa pili kulia) ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi jijini Dar es Salaam leo.
No comments