LGs WASHUSHA BEI ZA BIDHAA ZAO
Dar Es Salaam, Mei 2022, Kampuni mashuhuri kwa uuzaji wa bidhaa zinazotumia umeme ya LG Electronics East Africa imetangaza kuzindua Kampeni ya " LGs Something Better " kote nchini inayolenga kuboresha uzoefu wa ununuzi kwa wateja.
Kampeni hiyo, inatarajia kuendelea hadi tarehe 12 Juni 2022 kwa lengo la kuwapa wateja punguzo la hadi 20% kwa bidhaa zilizochaguliwa pamoja na thamani na manufaa zaidi kwa wateja wanaonunua bidhaa kutoka kwa maduka ya chapa ya LG.
Kwa punguzo la ofa, wateja wanatarajiwa kuokoa kuanzia shilingi 50,000/= hadi kufikia Tsh 1,000,000/= katika kipindi cha wiki tano zijazo katika bidhaa zote katika kategoria ya Burudani , Vifaa vya Nyumbani na Viyoyozi vya Makazi.
Akitoa maoni yake kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema,
Wanunuzi wamehakikishiwa kupata punguzo kubwa la hadi Tsh 539,200/=kwenye jokofu za LG Instaview 668(L), na Tsh 225,000/= kwenye jokofu la LG Instaview 544(L). Kwenye mashine za kufulia zinazotolewa, punguzo linaanzia Tsh 100,000/= hadi Tsh. 300,000 kwa mashine za kufulia ya 8Kg hadi ya 15Kg / dryer. LG microwaves, Neo Chef 20L, 23LNeoChef na 42L Neo Chef zote zina punguzo la kati ya Tsh 81,600/= na TZsh 122,800/=
Kufahamu zaidi kuhusu kampeni hii kabambe tafadhari tembelea mitandao ya kijamii ya LGs East Africa.







No comments