Breaking News

Tanzania Commercial Bank yakabidhi msaada wa jengo la darasa na choo wilayani Muleba, Kagera


.com/img/a/Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa: Faustin Kamuzora (wapili kushoto), akikata utepe wakati akikabidhiwa msaada wa jengo la madarasa 2  lililokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) , matundu ya Vyoo 2, pamoja na Madawati 50  Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika katika Shule ya Msingi Kitunga iliyopo wilaya ya Muleba mkoani Kagera (kushoto), ni Mkurugenzi wa Biashara na Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank, Adolfina William, (wapili kulia) ni Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki hiyo, Muondakweli Kaniki, pamoja na Mkuu wa Shule hiyo, Hashim Kibaiza, 

.com/img/a/


Mkurugenzi wa Biashara Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolfina William,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa jengo la madarasa, Vyoo, pamoja na Madawati mapya 50 lililokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika katika Shule ya Msingi Kitunga iliyopo wilaya ya Muleba mkoani Kagera kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia zaidi kiasi cha shs milioni 36 kukamilisha ujenzi wa madarasa Madawati pamoja na choo.

.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/
.com/img/a/

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof Faustin Kamuzora amewataka wazazi na wakazi wa Mkoa wa Kagera kusaidiana na serikali katika kutatua changamoto za walimu.

Hayo ameyasema wakati wa kukabidhiwa ukarabati wa madarasa, madawati na Choo cha matundu mawili kilichojengwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) kitakachosaidia kuboresha mazingira rafiki ya walimu kufundisha.

Prof Kamuzora amesema, wazazi na walezi wengi wa watoto wamesoma katika shule hiyo ila walimu wamekuwa na changamoto ya mazingira ambayo si rafiki na inaweza kupelekea walimu hao kuondoka na kwenda sehemu zingine.

“Walimu hawa wakiondoka tutakosa wa kuwafundisha watoto wetu, nyie wazazi wengi mmesoma hapa na mtu aliyesoma miaka ya nyuma akija hapa atapashangaa ila tusiwaachie serikali peke yake ila tushirikiane pamoja na wadau wa elimu pia,” amesema Prof Kamuzora.

Amesema, Benki ya TCB wamekuja na kujenga choo ila hii isiwe mwisho katika kutoa msaada bali walimu pia wanahitaji elimu ya fedha sababu wengi wamekuwa wanaingia katika mikopo inayowadidimiza kimaslahi.

Aidha, Prof Kamuzora ameitaka elimu ya fedha kuanza kutolewa mashuleni ili wanafunzi waanze kuwa na uelewa mkubwa na itawasaidia baadae.

“Na kwa upande wa walimu, haimaanishi ndio unajua kila kitu nao ni muhimu kuwa uelewa juu ya elimu ya fedha,”Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolphina William amesema wananchi wa Kijiji cha Msole wameweza kufurahia mradi wa kukarabati madarasa, kukabidhi madawati na walimu kupata choo cha kisasa.



Amesema, mradi huo uliofanyika katika Shule ya Kituga umeweza kugharimu kiasi cha Milioni 36.3 hadi kukamilika kwake.



“Tanzania Commercial Bank imekuwa inatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii na mwaka huu tumetenga takribani Milioni 500 na kujikita zaidi katika sekta ya elimu na afya,” amesema Adolphina.


Kwa upande wa Mkuu wa shule Hashim kibaiza ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kufanikisha mradi huo ambao utaenda kuboresha mazingira bora ya walimu katika kuinua taaluma.

Ameomba wadau mbalimbali kuiga mfano kwa Tanzania Commercial Banki ili kuendelea kujikita katika kusaidia jamii ikiwemo shule yao ya Kitunga.



Tanzania Commercial Bank imekabidhi ukarabati wa madarasa mawili, ujenzi wa choo cha walimu pamoja na kuchangia madawati 50 katika shule ya Msingi Kitunga iliyopo Muleba, mkoani Kagera mradi umegharimu Milioni 36,274,500 pesa za kitanzania.

No comments