RC MAKALLA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTORUDI NA KUFANYA BIASHARA KWENYE MAENEO WALIYOHAMA
- Asema Serikali itatumia sheria kuyalinda maeneo hayo na kurudi kufanya biashara katika maeneo hayo ni kosa.
- Awataka Wamachinga wengi Wajitokeze kupata nafasi Machinga complex.
- Atangaza nafasi 2,000 na route Za magari ya Kariakoo kufika machinga complex na masoko mengine mkoani DSM.
- Asema zoezi hili ni endelevu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Katika kuyalinda maeneo walipoondoka Machinga Serikali itatumia Sheria kwa Wote walioondoa Vibanda na kufanya Biashara Chini.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Maeneo mbalimbali walipohamia Machinga kukagua changamoto ili Serikali izitatue, RC Makalla amewataka Wafanyabiashara waliokuwa Kariakoo, Karume, Msimbazi na Katika ya mji kufika Machinga Complex ili wapatiwe nafasi ambapo mpaka Sasa nafasi zilizosalia ni 2,100.
RC Makalla pia amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuanza rasmi zoezi la Usafi kwenye maeneo yote walipoondoka Machinga na kuhakikisha yanalindwa yasivamiwe upya.
Aidha RC Makalla amesema Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zote zitakazoonekana kwenye maeneo walipopelekwa ili Biashara zifanyike na Wafanyabiashara wapate kipato.
Kwa mujibu wa sheria za miji na majiji zinaeleza kuwa kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ni kosa kisheria ambapo adhabu kwa anaefanya kosa hilo ni kifungo Cha mwaka mmoja na faini ya Shilingi laki tatu.
No comments