Chevron Brands International yaingia Mkataba na Tristar (AFAL) wa makubaliano ya utenegenezaji wa vilainishi katika Afrika Mashariki
Afisa wa Kimataifa wa Bidhaa za DRM Steve Hoffman (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Tristar Group Eugene Mayne, wakitia saini makubaliano ya BBDA kutoka maili mbali yenye lengo la kufanya kazi pamoja na kutengeneza na kusambaza na kuuza mafuta ya vilainishi ya CaltexTM katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Chevron Brands International yaingia Mkataba na Tristar (AFAL) kwenye leseni ya vilainishi na makubaliano ya utenegenezaji katika Afrika Mashariki.
- Mkataba mpya utaimarisha vilainishi vya Caltex kuongezeka Afrika Mashariki
(Dar es Salaam, Tanzania) Septemba 15, 2021: Kampuni ya Chevron Brands International LLC (Chevron) na AFAL Manufacturing Limited (AML) iliyopo chini ya Tristar Group, wameingia makubaliano ya muda mrefu ya kutengeneza na kusambaza na kuuza mafuta ya vilainishi ya CaltexTM katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Pamoja na kuingia kwenye mkataba huu, Chevron imeimarisha uwepo wake ambao tayari unakua katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kukabidhi leseni ya shughuli zake kwa AML.
Vilainishi vya mafuta vya chapa ya Caltex, vimekuwa vikipatikana katika nchi za Afrika Mashariki tangu mwaka 2013 vikisambazwa na kwa makubaliano na Africa Fuels & Lubricants Ltd (AFAL), pia ya Tristar Group. Kuaminiana na kuridhika kutoka kwa ushirikiano huu uliofanikiwa, ilikuwa ni sababu kubwa katika utambuzi wa kuingia makubaliano ya leseni ya muda mrefu. Kwenye upeo huu mpya, Chevron itatoa teknolojia inayoongoza ulimwenguni, na AML itachanganya, kuuza, na kusambaza vilainishi vyenye nembo ya Caltex kupitia mtandao wake mpana na kuingia katika soko la ushindani Afrika Mashariki.
“Chevron ina historia Afrika Mashariki, na tumejipanga katika miongo saba na tulianza ushirikiano na AFAL tangu mwaka 2013. Zaidi ya miaka nane, uhusiano wetu na AFAL umekuwa kwa namna moja hadi nyingine, na tunafurahia kuanza makubaliano mapya na AML, ambayo yatasaidia bidhaa za Caltex kusambaa maeneo yote ya Afrika Mashariki. Makubaliano haya yatajumuisha kukua na kusambaa kwa bidhaa hizo,” alisema Douglas Rankine, Meneja Mkuu wa Mafuta na Vilainishi Mashariki ya Kati na Afrika. “Pande zote mbili zilijitahidi wakati wa janga la korona na kuafikia mkataba huu, hivyo kuonyesha uhusiano ulioboreshwa unaotegemea uaminifu, uadilifu na utendaji.”
Kufanikiwa kwa makubaliano haya ya leseni na kuongezeka kwa mahitaji ya vilainishi katika mikoa, kulikuwa na sababu kuu katika kujenga zaidi uhusiano kati ya Tristar Group na Chevron, na itatambua kuingia katika soko jipya la Tanzania kama soko la AML.
Uhusiano huu wa kimkakati wa muda mrefu ni kielelezo cha kujitolea na uhakikisho wa Chevron kwa wateja, katika masoko ya Afrika Mashariki kutoa bidhaa bora na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya eneo hilo kupitia ushirikiano wa Chevron na AML katika soko la vilainishi vya Afrika Mashariki.
AML ina uhakika kuwa hatua hii itawezesha chapa ya Caltex kupata sehemu kubwa ya soko katika eneo la Afrika Mashariki kwa kutumia faida za gharama na ushirikiano wa mchanganyiko wa ndani.
“Kuchaguliwa na Chevron kwa jukumu hili muhimu ni onyesho la kujiamini katika uhusiano wa muda mrefu kati ya Chevron na Tristar Group tangu AFAL ilipopewa makubaliano ya usambazaji wa vilainishi na Chevron mwaka 2013, na itatumika kama sehemu ya uzinduzi wa vilainishi vyenye asili ya Caltex kupanua mauzo katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tuna hakika kuwa uchanganyaji wa ndani ni hatua inayofaa kwa biashara hii kubaki kuwa na ushindani, na hatutaokoa juhudi yoyote kuimarisha msimamo wa chapa ya Caltex Afrika Mashariki,” alisema Mtendaji Mkuu wa Tristar Group, Eugene Mayne.
Tristar ni Kampuni ya Biashara ya Kimataifa ambapo Makao Makuu yake ni Dubai, ambayo inatoa suluhisho na vifaa vya mafuta kwa wateja pamoja na kampuni za kitaifa na kimataifa, na mashirika ya serikali. Pia inajumuisha vifaa vya nishati katika usafirishaji wa nchi kavu na majini, maghala maalum, mashamba ya mafuta, biashara ya mafuta ya ndege na shughuli za usambazaji wa mafuta.
AML imejitolea kutengeneza vilainishi vya hali ya juu kulingana na viwango vya Chevron na imejitolea kushughulikia mahitaji ya wateja na matarajio ya soko yanayozidi kuongezeka nchi za Afrika Mashariki.
Pamoja na uhusiano huu wa kimkakati, Chevron na Tristar Group, wanawekeza zaidi kufikia kuongezeka kwa mahitaji ya vilainishi vyenye asili ya Caltex, ambayo inashughulikia sekta ya watumiaji, biashara na viwanda katika eneo lote la Afrika Mashariki.
No comments