WAZIRI GWAJIMA AZINDUA BARAZA JIPYA LA NACONGO ATOA MAAGIZO
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth
Gwajima, akizungumza wakati akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa
la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai
10, 2021 jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt.John Jingu, akizungumza
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya Dkt. Doroth Gwajima kuzungumza na
kupokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya
kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya uchaguzi Wakili Flaviana Charles, akisoma taarifa kuhusu
mchakato wa uchaguzi wa baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, wakati akipokea taarifa na kuzindua Baraza
la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika
leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth
Gwajima, akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika
Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya
uchaguzi Wakili Flaviana Charles, iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini
Dodoma.
Baadhi
ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, (hayupo pichani)
akizungumza na kupokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika
Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021
jijini Dodoma.
Mwenyekiti
Mpya wa NaCoNGO, Bi.Lilian Badi, akizungumza wakati wa kupokea taarifa
pamoja na uzinduzi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
(NaCoNGO) hafla iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Uratibu wa NGOs Dkt.Richard Sambaiga, akizungumza wakati wa
kupokea taarifa pamoja na uzinduzi wa Baraza la Taifa la Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) hafla iliyofanyika leo Julai 10, 2021
jijini Dodoma.
WAZIRI
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth
Gwajima, akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kupokea na kuzindua
Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO)
iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.
Na: Mwandishi wetu, DODOMA | WAZIRI
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima
amelitaka Baraza la la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCONGO)
kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo pamoja na kuzingatia
Sheria, kanuni, na miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya
waliowachagua.
Hayo
ameyasema leo, Julai 10, 2021 jijini Dodoma wakati akipokea taarifa na
kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa yakiserikali (NaCONGO),
Waziri Gwajima amelitaka Baraza hilo kufanya kazi weledi, uadilifu na
uzalendo.
“Nitoe
wito kwa viongozi na Wajumbe kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na
uzalendo pamoja na kuzingatia Sheria, kanuni, na miongozo iliyopo ili
kukidhi matarajio ya waliowachagua na Jamii ya watanzania kwa ujumla,” amesema.
Waziri
Gwajima amesema hana shaka na uongozi mpya kwani wataweza kutoa ratiba
mapema baada ya miaka mitatu uchaguzi ufanyike lini.
“Mmesema
tangu mwaka 2019 lilikuwa mfu sasa sijui tulikuwa tunafanyaje
kazi,Baraza hili nimeliamini sina Shaka na weledi,haiba yenu na mtasema
haraka lini uchaguzi ufanyike baada ya miaka mitatu,” amesema
Amesema Baraza hilo lilifanya uchaguzi mwaka 2016 ambapo mara baada ya hapo waliokuwa viongozi waligoma kufanya uchaguzi.
“Mimi
nasema baraza hili liligoma sasa tuwaache ninyi tizameni mbele hao
waliogoma mungu anawaona.Kutokufanyika kwa uchaguzi kunasababisha baadhi
ya Vyombo vishindwe kufanya kazi,” amesema.
Amesema viongozi wa Kamati ya mpito wamefanya kazi nzuri kwani lilikuwa mambo yalikuwa ni mazito.
“Nitoe shukrani zangu za dhati kwa kusimamia zoezi hili,Tunautambua umuhimu wenu hivyo tunawapongeza sana,” amesema.
Waziri
Gwajima amemtaka Mwenyekiti wa Baraza hilo, Lilian Badi kusimamia mambo
yaende vizuri huku akidai kwenye mambo ya fedha Mayuda huwa
hawakosekani.
“Baraza hili ni zito simama kwenye nafasi yako kwenye pesa mayuda hawakosekani,” amesema
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt.John Jingu
ameipongeza Kamati ya mpito kwa kusimamia vizuri uchaguzi.
“Nilikuwa
na wasiwasi mwezi mmoja utatosha Leo tunathibitisha kweli umetosha ila
watanzania wana matumaini makubwa nendeni mkasimamie Sheria na muwe
waadilifu,” amesema.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti mpya wa NaCONGO, Lilian Badi amesema wanaahidi
kufanya kazi kisayansi na kwa uadilifu mkubwa ikiwa ni pamoja na
kuwajibika ambapo amedai wamedhamiria kuona NaCONGO inarudi katika ubora
wake.
Amesema watakuwa mabalozi wa msajili katika Wilaya kwa kuhakikisha NGO’s zinafuata taratibu na sheria katika kujiendesha.
Pia, amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ambapo wameomba kuonana na Rais ili waseme kile ambacho wanacho.
“Muda
wa kuleta sintofahamu hatuna sisi tunataka kutoa Mchango kwa Taifa letu
ila tunaomba (mgeni rasmi) Mwambie Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan
tunampenda na mama yetu sio mgeni kwenye hii tasnia ya NGO’s,” amesema.
Awali,
Mwenyekiti wa Kamati teule ambayo ilisimamia uchaguzi, Flaviana Charles
amesema mara baada ya kuchaguliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Doroth Gwajima June 7 mwaka huu
walihakikisha uchaguzi unafanyika katika Mikoa 26 na Wilaya 139 kwa
kushirikiana na Ofisi za Msajili.
Amesema
katika chaguzi hizo walisimamia kanuni na vigezo ikiwemo mgombea kuwa
mfanyakazi wa Shirika ambalo limekidhi vigezo vya NGO’s, kuwa raia wa
Tanzania, kutokuwa na rekodi ya makosa ya jinai pamoja.
Mwenyekiti
huyo ametoa wito kwa baraza jipya kutengeneza ratiba mapema ya uchaguzi
ujao kwani Tanzania ni kubwa, kutengeza kanuni mpya kwani za mwaka 2016
zimepitwa na wakati, kuwe na mfuko wa fedha, kutafuta wafadhili ili
waweze kujiendesha, baadhi ya Mikoa iwe na wawakilishi wengi kwani ni
mikubwa akitolea mfano Mkoa wa Dar es salaam.
No comments